Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa na QT.

Jumla ya watahiniwa waliofaulu kwa Mujibu wa Matokeo hayo ni 23520 kuanzia daraja la I hadi la IV huku katika mchakato huo wasichana waliofaulu katika mchakato huo ni 7178 na wavulana ni 16342.Aidha Waziri Kawambwa amesema kuwa waliofaulu kwa daraja la kwanza ni 1641, daraja la pili ni 6495 na daraja la tatu ni 15426 na waliofeli ni 24903.

Shule bora ni pamoja na St. Francis Girl ya Mbeya, Marian Boys ya Bagamoyo, Feza Boys Dar es Salaam, Marian Girls Bagamoyo na Simini,hizo ndizo zilizopo kwenye tano bora huku shule nyingine ni Kanosa, Jude, St. Mary.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Asnte Mh.Kawambwa.

    KWENU BARAZA LA MITIHANI(NECTA).Matokeo kwenye website yenu ni kitu kizuri sana.Nawapongeza sana kwa hilo lakini kwanini msipange majina ya shule kwa ALPHABETI??.Yaani mtu unatafuta shule hadi macho yanauma.Wape kazi vijana wa IT wako wengi mtaani hawana ajira mtaani.

    David V

    ReplyDelete
  2. Bofya kwanza wewe , ukishayaona ndio nasi tubofye

    ReplyDelete
  3. sasa walio feli mbona namba yao ni kubwa zaidi hata walio fanya mtihani..je hii ni typo error au ndiyo report kamili

    ReplyDelete
  4. Asante kutupa taarifa, ila hizo link za baraza mbona zote hazifanyi kazi??

    Naelewa wanaopenda kuangalia matokeo tuko wengi ila hata kufungua page ya kwanza ni shida??? jamani

    ReplyDelete
  5. mbona matokeo yenyewe hatuyaon???????????????????? tunaona ya miaka iliyopita tu

    ReplyDelete
  6. Wakiofaulu Div I mpaka Div IV ni 23,520 na waliofeli ni 24,903.

    Hivyo asilimia ya watahiniwa waliofaulu ni 48.5% na waliofeli ni 51.43%.

    Taarifa hii inasemazaidi ya nusu ya watahimiwa wamefeli.

    Tunaomba takwimu za ufaulu wa watahiniwa wa kidatu cha nne miaka ya 1980, 1990 ili tuone kama kuna maendeleo ya kielimu kwa kutumia asilimia ya ufaulu wa wanafunzi na kama hali inaporomoka tujiulize ni kwa nini?

    ReplyDelete
  7. Mm jamani hiyo Website ya matokea kanyaboya maana imewekwa lakini kufunguka kwake sijui hadi YESU atakaporudi.

    ReplyDelete
  8. Labda sijui mahesabu jamani au ni macho yangu. Ukijumlisha waliofaulu
    Daraja la kwanza 1641
    Daraja la pili 6495
    Daraja la tatu 15426
    Jumla ya waliofaulu ni 23562. Tunaambiwa waliofaulu ni 23520 sasa hao 42 wanetokea wapi?

    ReplyDelete
  9. Matokeo ndivo yalivyo au usahishaji mbaya? Kuna shida gani? wanafunzi wabovu? au waalimu wabovu au hawakuandaliwa vizuri, au vitendea kazi? au ni vituko gani hivi? mbona sijaamini macho yangu?

    ReplyDelete
  10. Someni vizuri tangazo. Kweli mchambuzi wa hapo juu, waliofeli ni 51.34%. Halafu Bunge likiambiwa mfumo wa elimu Mbovu wanachachamaa. Ilhali takwimu ziko wazi. Matokeo ya miaka iliyopita, ndenda ktk website ya NBS. Kila mwaka unaposonga kufeli kunazidi.Hawa watoto watakuwa wageni wa nani katika hii karne ya Info Tech??? Uongozi kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  11. Mdau wa Sita hapo juu anony wa Mon Feb 18, 09:00:00 pm 2013

    ..Tunaomba Matokeo ya Miaka ya 1980 na 1990 ili tulinganishe!

    Mdau kwa kweli Kiwango cha Ubora wa Elimu nchini kinazidi kuzama Kaburini!

    Tukumbuke usemi usemao ya kuwa Kuelimika sio kuvuka Vidato au Kufaulu sio uwezo wa kujibu maswali mengi ya Mitihani kwa Ufasaha bali KUELIMIKA NI KUPOKEA MTAALA ULIO KIDHI MAHITAJI NA KUHITIMISHA MLOLONGO WA MASOMO (SYLABUS COVERAGE)

    Tukilinganisha Matokeo ya Ufaulu wa Miaka ile 1980 na 1990 tutaona waliokuwa Wanafaulu ni Wachache isipokuwa wanakuwa wana Kiwango cha juu ktk Kuelimika kuliko Kufaulu kwa idadi kubwa ya Utitiri kwa Wanafunzi wa Miaka hii huku wakiwa na Kuelimika kuliko chini ya Kiwango.

    ReplyDelete
  12. Elimu nchini ipo Kaburini kitambo tu, ilikwisha fariki tokea mwaka 1997 ilipobadilishwa Mitaala kwa mara ya kwanza.

    Ndio maana hivi sasa tunashuhudia % asilimia kubwa za Ufaulu wa Mitihani huku Viwango vya Taaluma Kielimu hakuna kabisa!

    -Tumeshuhudia Mwanafunzi anafaulu hajui kusoma na kuandika!

    -Mwanafunzi anaandika akichanganya herufi kubwa na ndogo!

    -Mwanafunzi anaandika jina (tena kwa hati mbaya kabisa) ktk sehumu ya Namba ya Mtihani!

    Hivi kwa mazingira hayo hapo juu tuna cha kujisifu kuhusu Kiwango cha Elimu nchini???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...