Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitandaza kufanyika kwa tafrija maalum la harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,itakayofanyika Februari 22 kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam.ambapo malengo ni kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali.Mgeni rasmi katika Tafrija hiyo anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA),Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Kulia ni Meneja Masoko na Mauzo wa Serena Hoteli,Seraphin Lusala na kushoto ni Mwenyekiti Kamati ya Maandlizi ya Tafrija hiyo,Barbara Hassan.
Meneja Masoko na Mauzo wa Serena Hoteli,Seraphin Lusala akifafanua jambo kwa wanahabari juu ya tafrija hiyo.
Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi ya Tafrija hiyo,Barbara Hassan akizungumzia maandalizi yalivyofikia.Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Montage,Zainab Mkindi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...