Mkurugenzi  wa Kampuni ya QS Entertainment, Joseph Mhonda, amesema kuwa amejipanga imara kuhakikisha kuwa tamasha lao la ‘Tumaini Jipya’ linalotarajiwa kufanyika Machi 31 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, linagusa hisia za wengi kwa kushirikisha wakali mbalimbali wa muziki wa Injili nchini.

 Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mhonda alisema kuwa alisema kuwa tamasha hilo lina lengo la kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu kwenye jamii ikiwemo watoto yatima na kutarajiwa pia kufanyika katika mikoa mbalimbali baada ya kuzinduliwa mkoani Morogoro. 

 “Tamasha hili limeanzia Morogoeo lakini litaendelea kwenye m ikoa mingine ya Tanzania likiwa na lengo la kutoa tumaini kwa jamii, na mapato yatakayopatikana yatasaidia watu walio katika mazingira magumu” alisema Mhonda.

  Alisema katika tamasha hilo ambalo ni la aina yake kufanyika Tanzania, litapambwa na waimbaji wakubwa wa muziki wa Injili Afrika Mashariki ambao ni Bahati Bukuku, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’, Joseph Nyuki, Stara Thomas, Matha Mwaipaja, Sifa John, Chamwenyewe na Revina Steven.

 Mbali na waimbaji hao pia kutakuwa na kwaya mbalimali Rafiki Gospel Singers, Haleluya Kwaya, Victoria Kwaya na MTC . Mhonda alisema sambamba na kutoa burudani ya mziki kupitia waimbaji hao pia watakuwa na muda maalum wa kutoa elimu ya Ujasiriamali kwa watu wote, pamoja na mbinu za kufaulu mtihani kwa wanafunzi. 

 Kwa mujibu wa waandaaji hao, Tamasha la Tumaini Jipya, ni fursa pekee kwa wakazi wa Morogoro kuweza kujumuika na watu wengine duniani katika kusherehekea siku Kuu ya Pasaka.
 Stara Thomas, Martha Mwaipaja, Bahati Bukuku, Masanja Mkandamizaji kukamua Tamasha la Tumaini Jipya Morogoro
 Stara Thomas akiwa na wakali wengine wa muziki wa injili ambao watakuwapo kwenye tamasha la Tumaini Jipya na picha nyinginezo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...