HONGERA AZAM KWA USHINDI LIBERIA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaipongeza klabu ya Azam kwa ushindi wa mabao 2-1 ilioupata timu yake katika mechi ya raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho.

Mechi hiyo dhidi ya Barrack Young Controllers II ilichezwa jana jijini Monrovia, na timu hizo zitarudiana wikiendi ya Aprili 6 au 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Ushindi huo unaiweka Azam chini ya kocha wake Stewart John Hall katika mazingira mazuri ya kusonga mbele baada ya mechi ya marudiano. Bila shaka ushindi wa timu ya Azam pamoja na mambo mengine umechangiwa na klabu hiyo kujipanga vizuri.

Hata hivyo ushindi huo bado ni changamoto kwa wachezaji, benchi la ufundi na uongozi wa Azam kuhakikisha unajipanga vizuri kwa mechi ya marudiano kwa vile mpira wa miguu una matokeo ya aina tatu; kushinda, kutoka sare au kufungwa.

Msafara wa timu ya Azam unaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Blassy Kiondo unatarajiwa kurejea nchini kesho alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi.

TAIFA STARS TRAINING PROGRAMME
Taifa Stars itacheza mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka nchini Brazil dhidi ya Morocco. Mechi hiyo itachezwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Jumamosi, Machi 16- Wachezaji kuanza kuripoti kambini
Jumapili, Machi 17- Mazoezi Uwanja wa Karume- Saa 2 asubuhi
Jumatatu, Machi 18- Mazoezi Uwanja wa Karume- Saa 9 alasiri
Jumanne, Machi 19- Mazoezi Uwanja wa Taifa- Saa 9 alasiri
Jumatano, Machi 20- Mazoezi Uwanja wa Taifa- Saa 2 asub na saa 9 alasiri
Alhamisi, Machi 21- Mazoezi Uwanja wa Taifa- Saa 9 alasiri
Ijumaa, Machi 22- Mazoezi Uwanja wa Taifa- Saa 9 alasiri
Jumamosi, Machi 23- Mazoezi Uwanja wa Taifa- Saa 10.30 jioni

PONGEZI KWA UONGOZI MPYA TAFCA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika juzi (Machi 16 mwaka huu) mjini Dodoma.

Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TAFCA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia taaluma ya ukocha nchini.

TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya TAFCA chini ya uenyekiti wa Oscar Don Koroso aliyeibuka mshindi kwa kura zote za ndiyo baada ya kukosa mpinzani.

Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu kwa kuzingatia katiba ya TAFCA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.

Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA chini ya Ramadhan Mambosasa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.

Safu nzima ya uongozi wa TAFCA iliyochaguliwa inaundwa na Dk. Oscar Dan Koroso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti), Michael Bundala (Katibu Mkuu), Gabriel Gunda (Katibu Msaidizi), Dismas Haonga (Mhazini), Wilfred Kidao (mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF).

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji waliochaguliwa ni Jemedari Saidi, George Komba na Magoma Rugora.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. BADALA YA KUJIBU HOJA ZA MSINGI, MNAKAA MNATOA TAARIFA AMBAZO KWA KIPINDI HIKI HAMNA MAMLAKA YA KUZITOA KWASABABU MPO MADARAKANI KINYUME NA KATIBA.

    MNAWASINGIZIA FIFA KWAMBA WANATAKA KUIFUNGIA TFF ETI KWASABABU FIFA WAMEPATA TAARIFA KUTOKA KATIKA VYOMBO VYA HABARI KWAMBA ETI SERIKALI IMEIINGIRIA TFF KATIKA KAZI ZAKE ZA KIUTENDAJI ZA KILA SIKU.

    SIKU HIZI DUNIA NI KIJIJI, FIFA SIKU ZOTE HAIFANYI MAAMUZI AU HAITOI MAAMUZI YAKE ("AS INSTITUTION")ETI KWASABABU WAMESIKIA AU WAMEPATA TAARIFA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI AU UMBEYA/PROPAGANDA KUTOKA KWA KITU/MTU YOYOTE KWAMBA SHIRIRKISHO/CHAMA FLANI CHA MPIRA DUNIANI KINA TATIZO AU MZOZO/MGOGORO NA SERIKARI YAKE.

    SIKU ZOTE FIFA INAFANYA MAAMUZI YAKE KUTOKANA NA MALALAMIKO RASMI ("OFFICIAL CLAIM") KUTOKA KWA SHIRIRKISHO/CHAMA CHA MPIRA CHA NCHI HUSIKA DUNIANI ("OFFICIAL CLAIM")

    KWAHIYO INABIDI TFF WASEME UKWELI, JE WALILALAMIKA FIFA?
    AU WATUELEZE ZILE TAARIFA AMBAZO WANASEMA KWAMBA FIFA WATAIFUNGIA TFF WAMEZITOA WAPI!

    KWASABABU FIFA KWA KILA MAAMUZI WANAYOFANYA WANAKUWA NA KUMBUKUMBU NAYO!

    HOJA YA MSINGI AMBAYO TFF WANABIDI WAIJIBU SERIKARI (UMMA WA ATANZANIA), JE UTARATIBU AMBAO RAIS WA TFF NA KAMATI YAKE YA UTENDAJI WALIUTUMIA KATIKA KUFANYA MAREKEBISHO YA KATIBA YA TFF ULIFUATA UTARATIBU KAMA JINSI KATIBA YA TFF ILIVYOVYOKUWA INAELEKEZA?

    KITU CHA MSINGI KUJUA NI KWAMBA, SERIKARI HAIJAINGIRIA KAZI ZA KIUTENDAJI ZA KILA SIKU ZA TFF! ILA SERIKARI INAIAMBIA TFF KWAMBA MCHAKATO MLIOUTUMIA KATIKA KUFANYA MAREKEBISHO YA KATIBA YENU YA TFF ULIUKUWA NI KINYUME NA KATIBA YENU YA TFF KAMA JINSI ULIVYOAINISHWA KATIKA KATIB YENU YA TFF.

    KWAHERI!
    NI MIMI,
    MTANZANIA MPENDA HAKI NA UKWELI.

    ReplyDelete
  2. Jamaa wa Mon Mar 18, 05:51:00 pm 2013:

    Umeongea ukweli. Watu ndiyo hawakielewi hicho cha katiba. TFF lazima iitishe mkutano mkuu kubadilisha katiba,kama katiba yao yenyewe inavyosema ya TFF. Hawawezi kubadilisha sheria kati ya maisha na kusema hawana hela kwa hiyo wanafanya kwa barua. Kama ni gharama basi ingebidi wangojee mpaka watakapo pata nafasi kufanya hivyo. Nanakumbuka wakati wanapitisha huu mchakato wa kubadilisha katiba kwa barua kwa vile FIFA imewaambia, kuna mikoa mingi iligoma, lakini TFF ikafosi tu. Matokeo yake tunayaona sasa. Hiyo siyo Demokrasia,kwani hata mnyonge akisema ameonea ni kweli ameonea. TFF safari hii wamechemsha,kwani wenyewe inabidi wahahakishe kwamba hawapati mgongano na serikali. Na siyo kusema seriakli haitakiwi kuingilia mambo ya michezo. Yaani hapa auitaji digrii ya sheria bali ni kutumia busara

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...