Airtel yatosha yatua kwa kishindo mkoani Tanga Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea na utaratibu wake wa kufanya matamasha ya wazi yenye lengo la kutoa burudani pamoja na kuitambulisha huduma yake mpya ya AIRTEL YATOSHA kwa jamii ambapo mwishoni mwa hii Airtel ilifanya tamasha katika viwanja vya Tangamano mjini hapo.
 Akizungumza wakati wa Tamasha hilo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema "Airtel tumefurahishwa sana na umati wananchi wanaojitokeza kwaajili ya burudani lakini pia inatusaidia kuwajulisha wote habari njema za unafuu wa gharama za mawasiliano kupitia huduma yetu ya Airtel YATOSHA Tunawakumbusha kuwa YATOSHA ni huduma ya kudumu na inasaidia sana kupunguza gharama za mawasiliano kwa wateja wetu. 
Kujiunga na huduma hii ili ujipatie vifurushi vya SIKU au WIKI piga *149*99# "Binafsi nimeshangaa na kufurahi sana sana kwa uwepo wa kifushi cha TOSHA cha hadi shilingi 349" na najipatia dakika 25 kuongea bure du kweli hii Imetosha!" alisikika akisema Hassan Juma mkazi wa chumba geni mkoani Tanga mara baada ya uzinduzi huo wasanii mbalimbali wa kizazi kipya akiwemo Ney wa Nitego, Nadii, Fid Q, na Juma Nature akiwa na kundi lake walipanda jukwaani kutoa burudani mfululizo huku wananchi waliojitokeza wakifuatia burudani hiyo mwanzo mwisho
Kati ya vibao vilivyopigwa na wasanii hao na kuwavutia wakazi wa Tanga ni pamoja na kile cha 'nani kwamwaga pombe yangu kilichoimbwa na Madee toka kundi la Tip Top Connection, wakati wahudhuriaji wa tamasha hilo wengi wao walionekana kuvutiwa zaidi na msanii wa hip hop Ney wa mitego hasa kwa umahiri wake wa kupanga mistari na free style zake alipoachia free style. 
Airtel inaendelea kufanya uzinduzi wa huduma ya airtel yatosha kupitia matamasha ya burudani kwa ambapo baada ya tamasha la Dar es salaam, Morogoro, Chalinze na Tanga kupita airtel yatosha jumamosi na jumapili hii inahamia jijini Mwanza katika viwanja vya Furaisha ambapo wasanii wa bongo flava watatoa burudani bure

Masanii  maarufu kwa vichekesho Masele  wa kundi la vituko shoo toka Dar es salaam akitoa burudani kwa wakazi wa Tanga  wakati wa Tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel yatosha katika viwanja vya
Tangamano mkoani Tanga

Umati wa wakazi wa Tanga wamejitokeza kushuhudia burudani na kuzindua rasmi huduma ya Airtel yatosha mkoani Tanga katika viwanja vya Tangamano mkoani humo
Wasanii wa kundi la Toto afrika wakionyesha umahiri wao wa kucheza na moto jukwaani wakati wa tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel yatosha katika viwanja vya tangamano mkoani tanga mwishoni mwa wiki 
Masanii Erick wa kundi vituko shoo toka Dar es salaam akitoa burudani kwa wakati wa Tamasha maalum la uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel ya Airtel yatosha katika viwanja vya Tangamano mkoani Tanga


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...