THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

BREKING NYUUUUUZZZZZ:ANKAL AANZISHA BENDI YA MUZIKI

 Ankal na bendi yake aliyoipa jina la Orchestre les Libeneke akiwa mazoezini na vijana wake kwenye kambi ambayo kwa sasa jina kapuni kwa kuhofia wadaku. Tayari bendi hiyo ina nyimbo nne huku ikifanyia kazi mbili zaidi, kabla ya kuingia studio kurekodi. 

Akiongea na mwandishi wetu wa maswala ya burudani kwa njia ya simu, Ankal amesema ameamua kujiingiza katika muziki kwani umo ndani ya damu yake ambapo kaka yake mkubwa Ismail ni mmoja wa waanzilishi na wanamuziki wa awali wa Dar International ya Marijani Rajabu. Pia Ankal anasema anafanya sana mazoezi na Wananjenje na hivi sasa anakaribia kuhitimu kupiga drums. 

Hakupenda kuweka bayana bendi itazinduliwa lini na wapi, ila alisisitiza ni kabla ya SabaSaba mwaka huu. Hivi sasa anatafutwa producer mkali wa kurekodi nyimbo zao pamoja na video. Huenda wakamtumia tiketi Producer mkali Miika Mwamba aliko huko Sweden  aje ashurikiane na wakali wa nyumbani kufanya vituzzzz.
Ankal akiwa na kijana wake Omary Makuka ambaye naye alipigia Dar International. Kwa sasa wanakamilisha nyimbo mbili za mwishio kabla ya kuingia studio. Katika hizo sita mbili ni 'Remix' ya ngoma za 
Marijani Rajabu 'Mayasa' na 'Rosa Nenda Shule'


Kuna Maoni 56 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Uzinduzi lini na wapi? Ningependa kukuona unaimba.

 2. Anonymous Anasema:

  happy fools day

 3. Anonymous Anasema:

  APRIL FOOLS.....
  Asante kwa kuniamsha na joke ya mwaka ankal!!!

 4. Balozi Tsere Anasema:

  Saafi sana ankal tuko pamoja!

 5. Anonymous Anasema:

  Ni kweli Ankal, nimekuona live na bendi jana sikukuu ya Pasaka kule mbugani halafu Kibo Sounds wakapanda jukwaani kuwapeni muda wa kupumua baada ya bendi yako Orch Les Libeneke kulazimishwa kupinga muziki masaa sita bila mapumziko na wadau uliopagawa na kazi yenu nzuri, show ilikuwa siyo mchezo.

  lini bebdi yako itafanya collabo na Msondo Ngoma au Mlimani Park ili wadau wa Dsm nao wafaidi?
  Mdau
  Mtalii wa Ndani

 6. Anonymous Anasema:

  1 April safi sana

 7. Anonymous Anasema:

  Fools day... Thank you sir.

 8. Anonymous Anasema:

  hapa utawapata wengi ANKAL

 9. Anonymous Anasema:

  Good try Ankal.
  Siku ya wa..... hoyeeeee.

  Mwilima, NYC

 10. Anonymous Anasema:

  Bw. Michuzi leo ni siku ya wajinga dunia!!!

 11. Anonymous Anasema:

  Leo ni siku ya wajinga, wadaganye!

 12. Anonymous Anasema:

  Siku ya wajinga duniani

 13. Anonymous Anasema:

  HAHAHAHAHAHA DAH.. VERY SOON UNCLE UTAANZISHA CLUB YAKO YA MPIRA ( FC. LIBENEKE)

  BY TH WAY LEO NDO 1ST APRIL SIO???????????????????

 14. Anonymous Anasema:

  Hongera sana ankal,kwahiyo unakwenda kama Nyoshi William?anyway kwangu leo hujanipata.

  MDAU TOKA K'KOO

 15. Anonymous Anasema:

  kazi ipo

 16. Anonymous Anasema:

  April fools day. Well try not this time ingawa una sauti kama ya Michael Jackson but this sounds fake April fools day.

 17. Anonymous Anasema:

  kwikwikwi. hahahaha..mbavu zangu kwishnehy..
  2015 ntakubook kwenye kampen zangu za ubunge kwa tkt ya M4C. tafadhali usinisepe
  mdau USA

 18. Anonymous Anasema:

  Sikukuu ya wajingaaa, SIDANGANYIKI
  Willy

 19. Anonymous Anasema:

  Ankal haya sio mambo ya 1st April kweli? teheteheteheeee!!

 20. Anonymous Anasema:

  Siku ya wajinga Leo, Hanna cha bendi wala kwaya, producer wala dj, Sweden wala mbagala.

 21. Anonymous Anasema:

  Fools day ankal ujatupata hapo! Band na ankal wapi na wapi........camera zitaota kutu

 22. Anonymous Anasema:

  Tafadhali!!!!,tafadhali!!!!Ankal hatutaki wawepo wacheza show maana vijana wa siku hizi wa zama za dijitali hawana adabu hata kidogo maana nina hakika mapigo ya bendi yetu yatakuwa ni ya kiutu uzima ya zama za analoji.

 23. Anonymous Anasema:

  ANKAL APRIL MOSI NINI?

 24. Anonymous Anasema:

  April Fool!!!!!!!!!!

 25. Anonymous Anasema:

  April 1

 26. Anonymous Anasema:

  Sikukuu Ya ......

 27. Anonymous Anasema:

  leo mjomba umpati mtuuuuu

 28. Anonymous Anasema:

  1st April, fools' day!!!!1

 29. Anonymous Anasema:

  April fool!! Hamnipati ng'o nimewashtukia!!

 30. Anonymous Anasema:

  wajingaz day! Humpati mtu ankal

 31. Anonymous Anasema:

  Yes, one of the best April Fools prank I have seen so far!

 32. Anonymous Anasema:

  Hongera sana uncle Michuzi

 33. Anonymous Anasema:

  Ankal hiyo umpati mtu

 34. Anonymous Anasema:

  ankali sio mbaya kuchangamsha blog lakini tuangalie hizi skukuu tunazozishabikia zina faifa gani kwa sisi wabantu?

  hivi kweli sisi wabantu na skukuu za kuiga tunaendana au ndio kwenye msafara wa wanyama hata panya yupo?

  hizi skuu za wajinga hatuna haja nazo sisi wabantu tupiganie njaa zetu

  wenzetu wameshashinda hili game la maisha ndio ukaona wanakuwa na skuu za ajabu ajabu

  wenzetu hawana shida ya UMEME,MAJI,NJAA,ELIMU,MATIBABU,KAZI,MAKAZI,N.K

  Shukrani kwa kutuchangamsha lakini kiukweli tusizifate hizi sio zetu.

 35. Anonymous Anasema:

  Mhhhh!!!machale yamenicheza,SIKU YA WAJINGA.

 36. Anonymous Anasema:

  April fools!

 37. Anonymous Anasema:

  Pole ankal! kidogo umechelewa baba Sela mbona wenzio wameanzaga mapema sana ushindani utauweza na Banza, Ila pia nikupe hongera, angalau utasema ulijaribugi

 38. Anonymous Anasema:

  Leo ni April 1st? Nimekubamba!

 39. Anonymous Anasema:

  Mnh! Ankal, leo ni siku ya wajinga.

 40. Anonymous Anasema:

  HII NDIO MAANA YA MJASIRIMALI AU ENTREPRENEUR ankal unakipaji hiki

 41. Anonymous Anasema:

  I Hope sio April fools day

 42. Anonymous Anasema:

  april fools..hahaa ankaaaal

 43. Anonymous Anasema:

  ankal hujakamata hata mmoja! leo umekamatwa weye yakhe
  --bpm

 44. Anonymous Anasema:

  hongera lakini mbona unaimba huku umeshika simu?

 45. Anonymous Anasema:

  Fools day au?

 46. D LANOR Anasema:

  Ankal - Hongera, lakini siyo sikukuu ya wajinga hii

 47. Anonymous Anasema:

  Siku ya awnings

 48. Anonymous Anasema:

  April 1, everyone knows that.

 49. mugo Anasema:

  Ankal,judging by the date of this post;I think you are pulling my leg...Happy april fools' day..

 50. Anonymous Anasema:

  aaaaa ap-- foolish

 51. Anonymous Anasema:

  Happy Fool's day!!

 52. Anonymous Anasema:

  *APRIL FOOLS DAY*!!!!!

 53. Anonymous Anasema:

  ankal leo ni sikukuu ya wajinga...hujui kuimba, hujui kucheza, una aibu sana kusimama mbele za watu, mkeo hata kuruhusu, huna kipaji...kiufupi si mwanamziki..!!

  Hapi april fools!

  mdau
  uswis

 54. Anonymous Anasema:

  Ankal ! hongera sana sana,umepiga hatua kubwa sana sana,kila kitu kinawezekana,tunataka kuona vitu kama hivi vinavyodumisha na kuendeleza muziki wa dansi na utamaduni wa muziki wa dansi wa kiswahili.
  Safi sana,babu kubwa.
  wadau
  FFU ughaibuni

 55. Anonymous Anasema:

  Tukumbuke leo ni 1-04-2013 yaani siku ya wajinga duniani,msisahau siku hii ya leo