Ankal na bendi yake aliyoipa jina la Orchestre les Libeneke akiwa mazoezini na vijana wake kwenye kambi ambayo kwa sasa jina kapuni kwa kuhofia wadaku. Tayari bendi hiyo ina nyimbo nne huku ikifanyia kazi mbili zaidi, kabla ya kuingia studio kurekodi. 

Akiongea na mwandishi wetu wa maswala ya burudani kwa njia ya simu, Ankal amesema ameamua kujiingiza katika muziki kwani umo ndani ya damu yake ambapo kaka yake mkubwa Ismail ni mmoja wa waanzilishi na wanamuziki wa awali wa Dar International ya Marijani Rajabu. Pia Ankal anasema anafanya sana mazoezi na Wananjenje na hivi sasa anakaribia kuhitimu kupiga drums. 

Hakupenda kuweka bayana bendi itazinduliwa lini na wapi, ila alisisitiza ni kabla ya SabaSaba mwaka huu. Hivi sasa anatafutwa producer mkali wa kurekodi nyimbo zao pamoja na video. Huenda wakamtumia tiketi Producer mkali Miika Mwamba aliko huko Sweden  aje ashurikiane na wakali wa nyumbani kufanya vituzzzz.
Ankal akiwa na kijana wake Omary Makuka ambaye naye alipigia Dar International. Kwa sasa wanakamilisha nyimbo mbili za mwishio kabla ya kuingia studio. Katika hizo sita mbili ni 'Remix' ya ngoma za 
Marijani Rajabu 'Mayasa' na 'Rosa Nenda Shule'

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 56 mpaka sasa

 1. Uzinduzi lini na wapi? Ningependa kukuona unaimba.

  ReplyDelete
 2. happy fools day

  ReplyDelete
 3. APRIL FOOLS.....
  Asante kwa kuniamsha na joke ya mwaka ankal!!!

  ReplyDelete
 4. Balozi TsereApril 01, 2013

  Saafi sana ankal tuko pamoja!

  ReplyDelete
 5. Ni kweli Ankal, nimekuona live na bendi jana sikukuu ya Pasaka kule mbugani halafu Kibo Sounds wakapanda jukwaani kuwapeni muda wa kupumua baada ya bendi yako Orch Les Libeneke kulazimishwa kupinga muziki masaa sita bila mapumziko na wadau uliopagawa na kazi yenu nzuri, show ilikuwa siyo mchezo.

  lini bebdi yako itafanya collabo na Msondo Ngoma au Mlimani Park ili wadau wa Dsm nao wafaidi?
  Mdau
  Mtalii wa Ndani

  ReplyDelete
 6. 1 April safi sana

  ReplyDelete
 7. Fools day... Thank you sir.

  ReplyDelete
 8. hapa utawapata wengi ANKAL

  ReplyDelete
 9. Good try Ankal.
  Siku ya wa..... hoyeeeee.

  Mwilima, NYC

  ReplyDelete
 10. Bw. Michuzi leo ni siku ya wajinga dunia!!!

  ReplyDelete
 11. Leo ni siku ya wajinga, wadaganye!

  ReplyDelete
 12. Siku ya wajinga duniani

  ReplyDelete
 13. HAHAHAHAHAHA DAH.. VERY SOON UNCLE UTAANZISHA CLUB YAKO YA MPIRA ( FC. LIBENEKE)

  BY TH WAY LEO NDO 1ST APRIL SIO???????????????????

  ReplyDelete
 14. Hongera sana ankal,kwahiyo unakwenda kama Nyoshi William?anyway kwangu leo hujanipata.

  MDAU TOKA K'KOO

  ReplyDelete
 15. kazi ipo

  ReplyDelete
 16. April fools day. Well try not this time ingawa una sauti kama ya Michael Jackson but this sounds fake April fools day.

  ReplyDelete
 17. kwikwikwi. hahahaha..mbavu zangu kwishnehy..
  2015 ntakubook kwenye kampen zangu za ubunge kwa tkt ya M4C. tafadhali usinisepe
  mdau USA

  ReplyDelete
 18. Sikukuu ya wajingaaa, SIDANGANYIKI
  Willy

  ReplyDelete
 19. Ankal haya sio mambo ya 1st April kweli? teheteheteheeee!!

  ReplyDelete
 20. Siku ya wajinga Leo, Hanna cha bendi wala kwaya, producer wala dj, Sweden wala mbagala.

  ReplyDelete
 21. Fools day ankal ujatupata hapo! Band na ankal wapi na wapi........camera zitaota kutu

  ReplyDelete
 22. Tafadhali!!!!,tafadhali!!!!Ankal hatutaki wawepo wacheza show maana vijana wa siku hizi wa zama za dijitali hawana adabu hata kidogo maana nina hakika mapigo ya bendi yetu yatakuwa ni ya kiutu uzima ya zama za analoji.

  ReplyDelete
 23. ANKAL APRIL MOSI NINI?

  ReplyDelete
 24. April Fool!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 25. Sikukuu Ya ......

  ReplyDelete
 26. leo mjomba umpati mtuuuuu

  ReplyDelete
 27. 1st April, fools' day!!!!1

  ReplyDelete
 28. April fool!! Hamnipati ng'o nimewashtukia!!

  ReplyDelete
 29. wajingaz day! Humpati mtu ankal

  ReplyDelete
 30. Yes, one of the best April Fools prank I have seen so far!

  ReplyDelete
 31. Hongera sana uncle Michuzi

  ReplyDelete
 32. Ankal hiyo umpati mtu

  ReplyDelete
 33. ankali sio mbaya kuchangamsha blog lakini tuangalie hizi skukuu tunazozishabikia zina faifa gani kwa sisi wabantu?

  hivi kweli sisi wabantu na skukuu za kuiga tunaendana au ndio kwenye msafara wa wanyama hata panya yupo?

  hizi skuu za wajinga hatuna haja nazo sisi wabantu tupiganie njaa zetu

  wenzetu wameshashinda hili game la maisha ndio ukaona wanakuwa na skuu za ajabu ajabu

  wenzetu hawana shida ya UMEME,MAJI,NJAA,ELIMU,MATIBABU,KAZI,MAKAZI,N.K

  Shukrani kwa kutuchangamsha lakini kiukweli tusizifate hizi sio zetu.

  ReplyDelete
 34. Mhhhh!!!machale yamenicheza,SIKU YA WAJINGA.

  ReplyDelete
 35. April fools!

  ReplyDelete
 36. Pole ankal! kidogo umechelewa baba Sela mbona wenzio wameanzaga mapema sana ushindani utauweza na Banza, Ila pia nikupe hongera, angalau utasema ulijaribugi

  ReplyDelete
 37. Leo ni April 1st? Nimekubamba!

  ReplyDelete
 38. Mnh! Ankal, leo ni siku ya wajinga.

  ReplyDelete
 39. HII NDIO MAANA YA MJASIRIMALI AU ENTREPRENEUR ankal unakipaji hiki

  ReplyDelete
 40. I Hope sio April fools day

  ReplyDelete
 41. april fools..hahaa ankaaaal

  ReplyDelete
 42. ankal hujakamata hata mmoja! leo umekamatwa weye yakhe
  --bpm

  ReplyDelete
 43. hongera lakini mbona unaimba huku umeshika simu?

  ReplyDelete
 44. Fools day au?

  ReplyDelete
 45. Ankal - Hongera, lakini siyo sikukuu ya wajinga hii

  ReplyDelete
 46. Siku ya awnings

  ReplyDelete
 47. April 1, everyone knows that.

  ReplyDelete
 48. Ankal,judging by the date of this post;I think you are pulling my leg...Happy april fools' day..

  ReplyDelete
 49. aaaaa ap-- foolish

  ReplyDelete
 50. Happy Fool's day!!

  ReplyDelete
 51. *APRIL FOOLS DAY*!!!!!

  ReplyDelete
 52. ankal leo ni sikukuu ya wajinga...hujui kuimba, hujui kucheza, una aibu sana kusimama mbele za watu, mkeo hata kuruhusu, huna kipaji...kiufupi si mwanamziki..!!

  Hapi april fools!

  mdau
  uswis

  ReplyDelete
 53. Ankal ! hongera sana sana,umepiga hatua kubwa sana sana,kila kitu kinawezekana,tunataka kuona vitu kama hivi vinavyodumisha na kuendeleza muziki wa dansi na utamaduni wa muziki wa dansi wa kiswahili.
  Safi sana,babu kubwa.
  wadau
  FFU ughaibuni

  ReplyDelete
 54. Tukumbuke leo ni 1-04-2013 yaani siku ya wajinga duniani,msisahau siku hii ya leo

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...