Maeneo mbali mbali ya jiji la Dar siku ya leo yalikuwa hayapitiki kabisa kutoka na foleni kubwa ambayo haikufahamika ilianzia wapi,maana si njia za barabarani wala za mitaani zilizokuwa zikipitika.kila mahala kulikuwa na msongamano wa magari.zifuatazo ni picha za hali ilivyokuwa maeneo mbali mbali ya jiji la Dar mchana wa leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. kazi hii wapewe SUMATRA traffic wameshindwa

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2013

    Suala la Foleni ni utitiri wa idadi kubwa ya magari ingekuwa ni Mtaji tosha kwa Manispaa na Mamlaka ya Umma ya Leseni za Usajili wa magari kuvuna Fedha nyingi sana.

    Manispaa za Jiji hasa hii ya Katikati ya Jiji ya Ilala na Mamlaka ya Umma ya Usajili wa Leseni za magari, zilistahili kutoa Leseni za Usajili wa Magari (PLATE NUMBERS KWA RANGI 3 KAMA HIVI)

    Kitovu cha Jiji la Dar (Dar Es Salaam Zero Point) kinajulikana ni Mnara wa Saa wa Clock Tower Samora Avenue inapoanza.

    1.Ili mwendeshaji wa gari aweze kuingia hadi zero point hadi 1 Kilometer from Zero point ina maana ni kama hadi Faya na Kariakoo, Mwendeshaji alipe Usajili MKUBWA zaidi kama mfano Tshs. 3 Million kwa mwaka na kupewa rangi za Kibao cha gari kwa ruhusa ya eneo husika...MFANO BLUE PLATE NUMBERS.


    2.Ili mwendeshaji wa gari aweze kuingia hadi 2 Kilometers from zero point hadi 3 Kilometer from Zero point ina maana ni kama kutokea Faya na Kariakoo hadi Magomeni, Mwendeshaji alipe Usajili WASTANI zaidi kama mfano Tshs. 2 Million kwa mwaka na kupewa rangi za Kibao cha gari kwa ruhusa ya eneo husika...MFANO WHITE PLATE NUMBERS.

    3.Ili mwendeshaji wa gari aweze kuingia hadi 3 Kilometers from zero point hadi nje kabisa ya Jiji ina maana ni kama kutokea Magomeni hadi nje kabisa ya Jiji la Dar, Mwendeshaji alipe Usajili CHINI WA KILALA HOI zaidi kama mfano Tshs. 500,000 kwa mwaka na kupewa rangi za Kibao cha gari kwa ruhusa ya eneo husika...HIZIHIZI YELLOW PLATE NUMBERS.

    Asiyeweza Viwango hivyo aegeshe gari lake nhyumbani au awe analitumia siku za Mapunziko kama Mwisho wa wiki na sikukuu ambapo ni bure.

    Pia ,mwendo huo wa gharama utazingatia mtiririko wa magari kama yatazidi na VIWANGO PIA VINAPANDA ili kupunguza msongamano wa magari hadi katikati ya jiji.

    Miji mingi iliyoendelea Usafiri wa Mjini ni wa Halaiki mfano wa Mipango ya Mabasi yaendayo Kasi DART na Mipango kama hii ya Treni za MWAKYEMBE.

    Kama utataka kutumia gari lako binafsi inabidi ulipie kodi zaidi na kuchangia Manispaa kwa ziada ya Utajiri uliojaaliwa wa kutaka kuingia hadi katikati ya Jiji ukiendesha na kusumbua miundo mbinu ya Umma.

    Kwa utaratibu huo, NDIO SULUHISHO SAHKIHI LA MSONGAMANO WA MAGARI NA FOLENI ZA JIJINI !

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2013

    Mdau wa 3 anony Wed May 01, 02:19:00 pm 2013

    Hahahahaha!

    HILO NDIO SULUHISHO, mawazo haya wapelekewe SUMATRA na pia Meya Mstahiki Mhe. Jery Silaa ili atekeleze.

    Duhhh umepiga Pentagon, maana Wabongo wana maradhi mabaya sana ya sifa mfano wanachukulia umiliki wa magari kama ndio uwezo wa kifedha!

    Yaani huo mpango utawaumbua watu walio wengi italazimika waegeshe VITZ zao Magomeni na kupanda mabasi kuingia katikati ya Jiji!

    Si, mnaona?, ile tu gharama za kuwa na Leseni ya kuingiza garilako ukiendesha hadi kati kati ya Jini ni Tshs. 3 Million yaani nusu ya bei ya Vitz!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2013

    anon wa pili; kwa kipato hikihiki cha mtanzania au kwa ufupi unahamasisha watanzania waibe zaidi? maana ili kununua hayo magari wamedokoa kidogo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...