Promota Kinda Nangolo wa Namibia (kulia) akiagna na Rais wa IBF/Africa Onesmo Ngowi wakati akiondoka nchini humo kuelekea Botswana

Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi amewasili katika jiji la Gaborone, Botswana kupromoti ubingwa wa IBF wa Kimataifa katika uzito wa Bantam.  
Bondia wa Botswana Lesley Sekotswe na bondia mwenzake kutoka nchini Namibia Immanuel “Prince” Naidjala walitoka sare wakati wakishindania ubingwa huo katika pambano lililofanyika katika jiji la Windhoek, Namibia tarehe 20 Mei  mwaka huu.  
Ujio wa Rais Ngowi ulikuwa unangojewa na wadau wengi wa ngumi katika nchi hii tangu aitembelee Botswana mwaka 2002 wakati wa mpambano kati ya bondia wa Botswana Thuso Kubamang na Peter Malinga kutoka nchini Afrika ya Kusini.  
Rais Ngowi atakutana na viongozi wa serikali ya Botswana pamoja na wadau mbalimbali wa ngumi na safari yake itaanzia jiji kuu la Gaborone mpaka jiji la pili kwa ukubwa la Francistown ambako wadau wengi wa ngumi wanamsubiri kwa hamu.  
Nchi ya Botswana ni nchi yenye msingi mzuri sana wa ngumi za ridhaa lakini tatizo kubwa limekuwa ni namna ya kuwaendelza wanapofikia kikomo kwenye ridhaa. Kikao cha Ngowi na viongozi wa serikali wa Botswana kitaweka msingi mzuri wa namna ya kuwaendeleza mabondia wa Botswana. 
Botswana ni nchi inayopakana na Namibia kwa hiyo mpambano wa Sekotswe na Naidjala unategemewa kuwa na wapenzi wengi wa ngumi kutoka katika nchi hizi mbili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...