Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania nchini Ujerumani Bw. Mfundo Peter Mfundo (pichani) anayofuraha kubwa kuwakaribisha watanzania na marafiki  wa Tanzania kutoka pembe mbali mbali za Dunia katika maadhimisho ya Sherehe Ya Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani, zitakazofanyika mjini Koloni hapa ujerumani.siku ya juma mosi Tarehe 27.04.13 kuanzia saa :08:00 za mchana  hadi usiku wa manane.

Katika sherehe hio ambayo  imedhaminiwa na Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kushirikiana na culture center ya sarakasi. Die Zirkus Fabrik,  kutakuwa na maonyesho ya bidhaa za Tanzania,  na atakayependa anaweza pia kununua bidhaa hizo. Ngoma za asili kutoka TanzaniaMwanamuziki Kongwe Bi.Tabia Mwanjelwa naye atakuwepo,  Msanii wa Bongo Flava Shah Smooth mwenye maskani yake  Dublin,. Kikundi cha Sarakasi kitafanya mavitu yake Live ! na  mwisho watanzania na wageni wote watapata Fursa ya Kuduarika na midundo  kutoka Tanzania kupitia DJ Sudi Mnete wa DW.
Akihojiwa na vyanzo vyetu vya habari mwenyekiti Bw Mfundo Alisema, Madhumuni ya sherehe hiyo sio tu kusherehekea siku kuu ya muungano pekee, bali ni kutimiza moja ya maazimio ya UTU la kuwakutanisha Watanzania wanaoishi nchini humo na kutangaza utamaduni wetu wa Tanzania kwa wenyeji wetu hapa Ulaya. Aliendelea kufafanua kwamba moja ya Agenda ya UTU ni kuhakikisha Watanzania wanaoishi nchini Ujerumani wanakuwa pamoja kwa hali zote, wanashirikiana kwa karibu na kusaidiana. Aidha  pia kuhakikisha wasanii wanaoisha hapa ujerumani wanatangaza kazi zao hadharani na wanazitumia kazi hizo kujipatia manufaa zaidi.Hivyo katika sherehe hii (UTU) imealika wasanii mbali mbali kuja kuonyesha kazi zao. Mwenyekiti alimaliza kwa kuwashukuru wasanii na watanzania ambao tayari wameshajiandikisha kushiriki katika sherehe hiyo kubwa Mjini Koloni,
Umoja ni Nguvu!
KARIBUNI SANA MJINI KOLONI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Muungano wa Tanzania bara na visiwani?!

    ReplyDelete
  2. Wewe Mtoa maoni wa kwanza, unaonyesha sio Mtanzania ama hukusoma ktk Mtaala wa Elimu ya Tanzania, sasa ulitaka uwe Muungano wa Tanzania bara na wapi ?, na Burundi ulipotokea wewe?

    Hujui Tanzania ni Muungano wa Tanganyika(Bara) na Zanzibar na Pemba (Visiwani)?

    Ninyi ndio wapinga Muungano wenyewe kutokana na uulizaji wako wa swali.

    ReplyDelete
  3. UTU huko Ujerumani, ktk mchakato wa maadhimisho ya Sherehe za Muungano huko Mjini Cologne msisahau vitu hivi muhimu:

    1.Mashairi,Maigizo na ngonjera,

    Muandae ya kuwananga Mamluki na Wapinga Muungano ambao wengi wao waliopo huko Majuu si Watanzania tena wameshapoteza Uraia na sasa ni wabeba Maboxi na Wakimbizi.

    Muandae Mchezo unaoonyesha Jinsi Mapinduzi yalivyo fanyika Zanzibar Januari 1964 (huku Mkoloni wa KIARABU akipinduliwa) na halafu mwezi April-1964 ukafuatia Muungano.

    2.Watanzania safi na Wanamapinduzi, muandae NYUNDO na JEMBE za chuma kama alama ktk eneo la sherehe ili Wapinga Muungano waone wakileta ujinga nyundo itawashukia vichwani utosini !!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...