Katibu Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda (kulia) akiangalia picha ya nembo ya chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria aliyopewa na Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya wanajeshi 22 kutoka chuo hicho wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku tano.
Katibu Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda (kulia) akimkabidhi picha ya wamasai Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John (kushoto) wakati wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Kanali Anderson Msuya (kushoto) kutoka Jeshi la Wananchi la wa Tanzania (JWTZ) akiongea jambo na Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John wakati wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu walipoitembelea wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Mchezo leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wakimsikiliza Katibu Mkuu kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda (hayupo pichani) wakati walipomtembea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza Joyce Fisoo akielezea kuhusu kazi za bodi hiyo kwa wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria walipoitembelea wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Joyce Hagu ambaye ni Kaimu Mkurugenzi msaidizi Idara ya utamaduni.
Wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati walipoitembelea wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Wanajeshi hao kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku tano. Picha na Anna Nkinda – Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...