THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Afande mpinga kazi kwako

Kamanda Mpinga unaiona hii ya leo karibu na New Msasani Club Barabara ya Mwai Kibaki Road jijini Dar es salaam? Huyo dereva sio tu aliamua kupita katikati ya foleni bali pia alikuwa katika mwendo wa kasi na fujo huku akipiga honi. Mie mwenyewe kanikosa kunipiga pasi Kitetenesi changu....Wanaomjua wanasema dereva huyo hizo ndio zake na  hakuna wa kumgusa (ati hata wewe) kwa kuwa yuko 'Connected'. Je ni kweli jamaa yuko juu ya sheria??
Mdau Msasani Kwa Mwalimu


Kuna Maoni 7 mpaka sasa.

 1. Stuart Heddi Anasema:

  HEBU TUONGEE NA MAKAMANDA ILI KAMERA ZIANZE KUWA DILI YAANI TUANZISHE BLOGU LA USALAMA BARABARANI TU NA HAPO UKIPELEKA PICHA YA FAULO BARABARANI IKWA NI PAMOJA NA DALADALA KUPAKI NJE YA VITUO AKIKAMATWA NA KUPIGWA LIFAINI LAKE KAMA LAKI HIVI UNAPEWA ANGALAU 30,000/= TUONE KAMA HAWATAACHA!

 2. Anonymous Anasema:

  Wazo lako nzuri sana mdau wa kwanza, si wewe tu tena katika blog hiihii watu mbalimbali walishaleta mawazo kama hayo kwa matukio kama haya kwa upande wa mabasi yaendayo mikoani, nachelea kusema bongo mawazo yenye kujenga hawana haja nayo kaka,Walikuja watu wazuri wenye mawazo mazuri tena ya kizalendo leo wametuachia majonzi,wametutangulia,walishauri mengi yenye maslahi lakini walipuuzwa.

 3. Anonymous Anasema:

  Hiyo Costa ni ya mmoja wa Kamanda wa Polisi tena mkubwa nafikiri ni ya Mahita hizi

 4. Mnyalu Anasema:

  Nini 30,000? Mpelekeni pale Sumatra ofisi ya Mwalimu haouse wale jamaaa ni noma! hawana salie mtume, walinisulubu sana na Noah yangu na huwezi kuwashawishi.Angekoma ndugu

 5. Anonymous Anasema:

  Hata Mimi nimewahi kukumbana na dala dala hii siyo mara moja. Dreva huyu anaendesha kama ndio yeye tu katika barabara. Inasikitisha sana.

 6. Anonymous Anasema:

  Du jamani nilizani ni mie peke yangu mie nusu aniingize kwenye mtaro pale chama kisa basi la kigogo wa polisi, tafadhali tunaomba jeshi la polisi kikosi cha barabarani wamfuatilie dereva huyu mbona NANGA BOY mambasi ya mwenge posta mpaka kunduchi na yenyewe ni ya mzito ila angalia vijana wale walivyo na nidhamu barabarani.

 7. Anonymous Anasema:

  Mnapiga blah blah tuu... hata madereva wa magari mnatua hovyo hovyo... Kamanda Mpunga sio mwenye makosa; ameshatoa rai madereva wafuate sheria; ila mnakaidi hata huyu dereva(mwehu) anakaidi. Madereva mnatakiwa mjifikirie na kubadili tabia.