Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe ambae pia ni mdau kubwa wa Muziki hapa chnini,pia alikuwa ni mmoja wa wazungumzaji kwenye semini hiyo iliyohusu na  harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii,iliyofanyika mapema leo kwenye ukumbi wa hoteli ya African Dreams,nje kidogo ya mji wa Dodoma.kutakuwepo na kampeni ya matembezi ya hisani ya harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii yatakayofanyika kesho,wabunifu na wavumbuzi mbalimbali, mseto wa shuguli mbalimbali zitahusishwa.  Aidha pia mchana huu kutakuwepo na burudani hadhara ya sanaa za kisasa na za kitamaduni,mpira, chakula na bidhaa mbalimbali za kitanzania katika uwanja wa jamhuri .
 Mmoja wa wasemaji kwenye semina hiyo aliyejitambulisha kwa jina la   Patrick Ngowi  kutoka kampuni ya Helvetic Solar Contractors, akizungumzia fursa mbalimbali kuhusiana na mambo ya ujasiliamali na pia alielezea ni namna gani amefanikiwa mpaka kufikia kumilimiki lampuni yake binafsi kupitia fursa alizokuwa akikumna na nazo na kuzifanyia kazi vilivyo.
 Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akiuliza swali kwa Mh Zitto Kabwa kuhusiana na mambo mbalimbali ya ujasiliamali na namna ya kuzitumia fursa hizo katika kujikwamua kimaisha.
 Mh Zitto kabwe akimsikiliza mmoja wa washiriki wa semina hiyo alipokuwa akiulizwa kuhusiana na suala la fursa zinazopatikana kwa vijana na namna ya kuzitumia katika ujumla wa kujikwamua na ugumu maisha,ambapo watanzania wengi wamekuwa wakizilalamikia.

Mtangazaji wa clouds FM kupitia kipindi cha Power Breakfast-Gerald Hando akiikaribisha Meza kuu pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds Media Group unaokwenda sambamba na ujumbe wao thabiti kabisa  ulioitwa MADE IN TANZANIA,ikiwa na hamasa kubwa ya kuleta msingi wa fursa kwa watanzania, msukumo ikiwa ni kuwashawishi watanzania kuanza kuzifanyia kazi fursa hizi kwa umoja na maendeleo ambapo TWENZETU, inakuwa neno rasmi la mawasiliano.Kama vile haitoshi kutakuwepo na kampeni ya matembezi ya hisani ya harakati rasmi za vita dhidi ya uharamia wa kazi za wasanii yatakayofanyika kesho,wabunifu na wavumbuzi mbalimbali, mseto wa shuguli mbalimbali zitahusishwa  ikiwemo semina ya fursa kwa watanzania,burudani hadhara ya sanaa za kisasa na za kitamaduni,mpira, chakula na bidhaa mbalimbali za kitanzania zitapatikana uwanja wa jamhuri mapema leo mchana.
Mmoja wa wasemaji kwenye semina hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Zenno  Ngowi kutoka kampuni ya Tanzania Home Expo akizungumzia fursa mbalimbali kuhusiana na mambo ya ardhi,ujenzi,na mengineyo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria kwenye semina hiyo leo mjini Dodoma.


Mmoja wa wasanii mahiri wa Mashairi,Mrisho Mpoto akifafanua jambo kuhusiana na mambo mbalimbali katika suala zima la wasanii kujipa nafasi ya Fursa mbalimbali zinazojitokeza mbele yao na namna ya kuzifanyia kazi na kuziboresha zaidi.
Mhe Zitto Kabwe akiwasili kwenye ukumbini mapema leo kwenye hoteli ya African Dreams mjini Dodoma,Mh Zitto pia alikuwa ni mmoja wa wasemaji wa semina hiyo.
Pichani ni washiriki wa semina hiyo kutoka sehemu mbalimbali mjini Dodoma leo. PICHA ZAIDI INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2013

    MBONA ANALIA?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2013

    ANALILIA NCHI YAKE KWA JINSI ULIVYOIHARIBU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...