MAREHEMU PIUS WILFRED SHANGALI.

Ni Miaka 5 sasa tangu ulipotutoka ghafla alasiri ya tarehe 30/4/ 2008 huko nchini  Ujerumani.


Hakika ilikuwa ngumu sana kukubaliana na  taarifa za kifo chako kwani ni wiki 2 kabla ya taarifa hizo ulikuja kutusalimia hapa nyumbani Tanzania, Laiti tungejua ulikuwa umekuja kutuaga na hatutaonana tena. Mpendwa na kiongozi wa familia yetu, tunaamini umepumzika kwa amani, japo hatuko nawe kimwili lakini imekuwa vigumu mno kukusahau kulingana na umuhimu na nafasi uliyokuwa nayo kwenye familia yetu.

Unakumbukwa na Wazazi wako Mr & Mrs W. Shangali,dada na wadogo zako Suzy,Jane,Theophil,John,Christer na Bertha.  Umetuachia fumbo zito lakini kwa yote tunamshukuru Mungu kwani umetuachia mengi ya kuiga, Hekima zako, upendo, upole, uvumilivu vimebaki mioyoni mwetu na tutavienzi daima.

Tunaamini kukutana paradiso ya milele. upumzike kwa amani kaka Pius.
Jina la Bwana libarikiwe . Amen.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...