THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

KUTOKA MAKTABA YA GLOBU YA JAMII

Mnara wa Askari jijini Dar es salaam enzi hizi na hizi sasa.
Hii  ni kumbukumbu ya askari jeshi waliopigana katika vita ya kwanza ya dunia inayosimama kuangalia bandari ya jiji hilo. 
Ilizinduliwa mwaka 1927. Sanamu hiyo ya askari wa British Carrier Corps iliundwa Uingereza na mchonga sanamu Mwingrereza aitwaye James Alexander Stevenson ambaye katika sanamu hii katumia jina lake la kufikirika la “Myrander”. 
Kabla ya kupelekwa Dar es salaam sanamu hii ya Askairi ilioneshwa kwa muda jijini London katka Royal Academy. Kabla ya kuwekwa sanamu ya askari, mahali hapa palikuwa na sanamu ya Meja Herman von Wissman, gavana wa wakati huo wa German East Africa, iliyozinduliwa mwaka 1911. Waingereza walipoingia Dar es salaam mwaka 1916, waliibomoa sanamu ya gavana wa Kijerumani pamoja na zingine za Karl Peter na Otto vo Bismarck zilizokuwa hapo. Sanamu ya askari ya Dar es salaam ni moja kati ya tatu zilizozinduliwa wakati mmoja kati ya tatu zilizoweka katika mwaka huo wa 1927 sehemu za koloni ya Uingereza ya Afrika Mashariki (British East Africa). Zingine mbili zilikuwa Mombada na Nairobi.Kuna Maoni 6 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Awesome. Very educative.

 2. Anonymous Anasema:

  Asante kwa kutupatia historia hii.

  Uendelee kutuelimisha.

 3. Al Musoma Anasema:

  Kumbe kanzu fupi hazijaanza juzi!

 4. Anonymous Anasema:

  Ohhh ala kumbe ndio hivyo siyo?

  Sasa yote hayo na kuibomoa Sanamu ya wenzao ya nini?

  Ndio maana Mwingereza na Mjerumani ni kama Mzaramo na Mnyamwezi!

 5. Anonymous Anasema:

  Baada ya Talaka mara zote Mtalikiwa hukumbuka alipokuwa kwenye Ndoa!

  Kwa matatizo kama kushuka kwa Kiawango cha Elimu tunamkumbuka Mwingereza!

  Kwa uzembe ktk sehemu za Kazi tunamkubmuka Mjerumani na Kiboko Mkononi!

  Lakini kubwa ya yote kwa anayotufanyia Mwingereza na kutupangia (MPANGO WA NDOA ZA JINSIA MOJA KUWA SHARITI LA KUPEWA MISAADA YA MAENDELEO) ni bora wangerudisha Sanamu ya Meja wa Kijerumani Hermann Von Wismann!!!

 6. Anonymous Anasema:

  Eti, kumbe hawa wenye kanzu, kofia na mabaibui ndio wenye mji hapo.

  Sasa ni nani baadae amewasukuma hadi hawaonekani tena, ni haohao Waingereza au?

  Tafakuri!