THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Kutoka maktaba ya globu ya jamii

Septemba 1973 jijini Algiers, Algeria: Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika mazungumzo na Rais wa Uganda Field Marshal Iddi Amin Dadah pembeni mwa mkutano wa nchi zisizofungamana na upande wowote. Kushoto ni Mama Maria Nyerere na kulia ni Waziri wa Nchi za Nje Mhe John Malecela. 


Kuna Maoni 10 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  1.''Kutika kwa Debe ndani mshindo mtupu''

  2.''Kelele za jogoo awapo Tunduni bahati mbaya sana anakuwa hana uwezo wa kufungua Tundu ili atoke''

  Yaani Idd Amini muonekano wake , alivyokaa na alivyojifutua huku Kambarage akiwa amejikunja pembeni inaonyesha Mwamba ni Idd Amini!

  Lakini mwisho wa yote wanaingia vitani Tanzania na Uganda huku yeye Mwamba Idd Amini akijikuta anakwenda kuishi Uhamishoni SAUDI ARABIA hadi kifo chake!

  Yaani ngano hii ipo sawasawa na jinsi maisha yetu yalivyo kati ya WANYONGE na WABABE, mwishowe WANYONGE huibuka Kidedea mara zote wale wanaojifutua mwisho wao huwa mbaya, hugonga Ukuta na wakaumbuka!

 2. Anonymous Anasema:

  Haya wapi tulikosea hata vita ikatugharimu? Yumkini kuna kitu nyuma ya pazia la historia bado hakichafichuliwa kuhusu uhasama wa hawa jamaa. Sidhani kama ni Kagera tu. Any way yaliyopita si ndwele, tusameheaneili maisha yasonge. Ahsante Ankal

 3. Anonymous Anasema:

  Mh ladba lakini sio kila siku wanyonge wanashinda. Kama ni ushindi wengine wanautegemea kwa Mungu kama utakuwepo vinginevyo dalili za kushindwa ziko wazi. Angalia kijogoo marekani kama marekani na mabepari weingine. wanavyosulubu na kuzipangia nchi changa jinsi ya kuendesha nchi zao kwa watakavyo wao.

 4. Anonymous Anasema:

  Very true, mwalimu`s body language was not a confident one, avoiding eye contact and talkinh without the facing nduli, mama maria had a defensive stance, nduli was confident and rather relaxed,this lasted until TULIVYO MLIMBA.

 5. Anonymous Anasema:

  Ni sawa anony wa mwanzo lakini kumbuka kwamba hadi leo ile mikanda tuliyoambiwa tuifunge kwa miezi 18 bado hatujaambiwa tuifungue zaidi ya miaka 30!! Na hii ndio consequence mbaya zaidi kwani inazidi kutubana vikali sana!!!

 6. Anonymous Anasema:

  Ni sawa anony wa mwanzo lakini kumbuka kwamba hadi leo ile mikanda tuliyoambiwa tuifunge kwa miezi 18 bado hatujaambiwa tuifungue zaidi ya miaka 30!! Na hii ndio consequence mbaya zaidi kwani inazidi kutubana vikali sana!!!

 7. Anonymous Anasema:

  Mtoa Maoni wa 3 mara zooote Dhalimu mwisho wake ni mbaya!

  Ndio maana hata wenyewe miongoni wa Wamarekani wenye akili na kufikiria hatma ya baadaye wanapinga vikali Sera mbaya ya Marekani ya kuendesha vita nje na kuingilia masuala ya nchi zingine.

  ''Opposing AMERICAN FOREIGN POLICY'' Kundi hili ktk Marekani ni kubwa na linazidi kukua la watu wasiotaka vita na Marekani kuiningilia masuala ya ndani ya nchi zingine.

  Hata Israel wapo wasiotaka mwenendo uliopo wa Israel kuhusu mataifa mengine na hasa Palestina.

  Maafa mengi yanayotokea ndani ya US na Israel kwa sasa yapo nyuma ya harakati hizi za kupinga FOREIGN PILICIES zao ktk nchi hizo.

  Ndio maana unaposikia mahala kumelipuliwa wakati mwingine Walipuaji wanakuwa ni wenyewe wahusika wenye nchi kama ishara ya kupinga Serikali zao juu ya Sera hizo.

 8. Anonymous Anasema:

  kuna moja ya video za idd amin katika interview zake aliulizwa kuhusu mwalimu nyerere idd amin akajibu kuwa mwalimu nyerere angelikuwa ni mwanamke basi angemuoa awe mke wake wa 5 dah kaazi kweli kweli.

 9. Anonymous Anasema:

  Amini bwana na tepe zake za vizibo vya: Cocacola, Fanta, mirinda, Vimto, pepsi, seven up, plisner, safari, konyagi, kilimanjaro nk. Kweli alikuwa mwana maigizo.

 10. Anonymous Anasema:

  Daudi na Goliati: Haki hatimaye hutawala, iweje! iweje!