Pichani juu na chini ni wafanyabiashara wa nyama ya mbuzi wakisaka wateja eneo la Mkata mapema jana jioni,ambapo mbuzi mzima humuuza kati ya sh.35,000/= mpaka 40,000/=.Pamoja na biashara hiyo kunoga eneo hilo vipi tatizo la kutozingatia afya ya mlaji?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2013

    Jamaniiiiii natumaini hakuna atakaye nunua nyama hizo zinazo tembezwa barabarani kama karanga maana ndo mwanzo wa magonjwa kulipuka!! Waapi waziri wa afya na kikundi chake akemee jamambo hili? Inamaana kunawatu wananunua ndo maana zinauzwa hapo barabarani sio? Watanzania aamkeni msinunue vitu bila kupimwa jamani? chondo chonde kuna kipindupindu, amoeba na typhodi kama magonjwa ya mlipuko!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2013

    Mdau wa kwanza, hicho kitoweo kinakwenda kupikwa kwa moto hivyo magonjwa unayozungumzia wewe watakuwa hawampati mlaji. Tatizo la nyama za kununua namna hiyo ni suala la uchinjaji ni muhimu kwa waumini wa Dini ya Kiislam. Pia inawezekana huyo sio mbuzi bali ni paa mwitu au mbwa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2013

    wewe unadhani chakula cha mama mtilie nyama wanapata wapi?Ndiyo hiyo mjomba wali na nyama chomaaaa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 20, 2013

    mdau wa mwanzo "penye mteja hapakosi biashara" midhali wako wanaonunua hiyo nyama wauzaji wataendelea tu kuuza bidhaa zao namna hiyo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 20, 2013

    Bahati nzuri ni kuwa INZI wa Vijijini angalau Kisayansi hawana maambukizi ya hatari kama hawa wa Mijini kwa SABABU HIZI HAPA CHINI ZA KISAYANSI:

    1.KINACHO ATHIRI KUPITIA KWA INZI NI UBEBAJI WAKE WA VIINI VYA MARADHI ANAVYOPATA INZI KUTOKANA NA MAHALA ANAPOKAA.

    2.VIJIJINI HAKUNA MIRUNDIKANO NA MAZALIANO YA UCHAFU KTK MAJALALA.

    3.MAJITAKA NA KUTUAMA KWA TAKATAKA KUNAWEKA MALIMBIKIZO YA VIINI VYA MARADHI.

    4.MFANO VISIMA VYA MAJI VYA MIJINI NI HATARISHI KWA SABABU MAJI YA VYOO YANAZUNGUKA MAKAZI HUKU UCHUJAJI WA TAKA UKIWA HAUKAMILIKI TOFAUTI NA VISIMA VYA VIJIJINI HAVIPO KATIBU NA MAZINGIRA YA MAKAZI.

    5.INZI WA VIJIJINI HULA MASALIA YA MAZAO KAMA CHAKULA HIVYO KUPUNGUZA ATHARI ZA VIINI VYA MARADHI NA VIINI HATARISHI, WAKATI INZI WA MIJINI HULA MABAKI YA MZUNGUKO WA TAKA ZA BINAADAMU NA MZUNGUKO USIOSAFISHIKA WA TAKA ZA VYANZO VINGINE.

    HIVYO HYGIENICALLY VIJIJINI KUNAKUWA SALAMA ZAIDI KULIKO MIJINI HATA INZI WAKE HAWABEBI VIINI VINGI NA HATARISHI KULINGANA NA MAZINGIRA YAO.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 20, 2013

    Nyama ya mbwa haina matatizo ila kidini tu.Nasikia jamaa huko kwenye njia ya mabasi, Alisha watu wali wa kuku, na kuku wake ni mabundi, nyangenyange na makunguru.If its digestable, eat it.Tomorrow is another day.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 20, 2013

    Nania kasema mie nanunua kwa kwenda mbele na sijawahi ona madhara yake kwanza bei che nenda vingunguti ukasikie bei.

    ReplyDelete
  8. manka-mwanzaMay 20, 2013

    eti hakuna atakayenunua labda wewetu ndio hutanunua kwa sbb huna hela, endelea kula hizo mboga zako unazonunua karaikoo zinazolimwa mto msimbazi zenye mbolea ya vinyesii na maji ya mikojo.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 20, 2013

    MKATA ndo wapi tena?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...