Mke wa Rais  na Mwenyekiti wa WAMA, Salma Kikwete (katikati) akisalimina na Mkurugenzi wa ITV, Joyce Mhavile na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited, Teddy Mapunda.
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Salma Kikwete (kulia) akizungumza na Uongozi wa Montage pamoja na wadhamini wa Harambee iliyoongozwa na Kampuni ya Montage kwaajili ya kuchangisha fedha kwaajili ya kusaidia matibabu ya Mama na Mtoto nchini Tanzania.
  Mkurugenzi wa ITV, Joyce Mhavile (kushoto)akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited, Teddy Mapunda kabla ya kukabidhi hundi kwa Uongozi wa WAMA.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Salma Kikwete akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 70 kutoka kwa Mkurugenzi wa Montage Limited, Teddy Mapunda ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo katika kuchangia Afya ya Mama na Mtoto. Fedha hizo ni sehemu ya michango ya wadau mbalimbali iliyopatikana katika harambee maalum iliyopendeshwa na Montage hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Fedha wa Montage, Zainabu Mkindi (wapili kushoto)na kulia ni Katibu wa WAMA, Daud Nassib. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...