Msanii mahiri wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA (pichani) ambae ni Balozi wa Chapa Vodacom amesema hadhi na heshima ya mwanaume katika jamii itakuwa na uzito mbele ya uso wa jamii kwa wao kuwa tayari kutafuta suluhu ya changamoto zinazoikabili jamii na wala si vinginevyo.
Mwana FA ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati wa kampeni ya kuelimisha jamii kuhusu fistula iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square kuelekea siku ya fistula dunaini Mei 23. 
Kampeni hiyo inadhaminiwa na kampuni ya Vodacom na Vodafone ya Uingereza ikiihusisha mikoa mbalimbali. 
Balozi huyo amesema ni wazi kwamba wanaume wamekuwa wamiliki wa maamuzi katika jamii huku wakitajwa kuwa nguzo ya familia lakini sifa hizo na mamlaka hayo yatakuwa na dosari kubwa iwapo hawatokuwa pia mstari wa mbele katika kuhakikisha jamii inapata suluhisho la matatizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...