Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto) akipokewa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha zinazofuata Kanuni za Kiislamu ‘NBC Islamic Banking’ cha Benki ya Taifa ya Biashara, Yassir Masoud alipokwenda kufungua semina ya siku moja kwa wanawake wajasiriamali waislamu iliyoandaliwa na NBC mjini Tanga leo. Katikati ni Meneja Tawi la NBC Tanga Deusdedit Mashalla.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa akifungua semina ya siku moja kwa wanawake wajasiriamali waislamu iliyoandaliwa na Benki ya NBC Kitengo cha Islamic Banking mjini Tanga LEO. Kulia ni Mkuu wa kitengo hicho, Yassir Masoud na kushoto ni Meneja Operesheni wa NBC Tawi la Tanga Kibibi Said Kibao.
Baadhi wa washiriki wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Benki ya NBC Kitengo cha Islamic Banking wakiwa katika semina hiyo jijini Tanga leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...