CHE MUNDUGWAO
--- 
MIMI NASHANGAA SANA JUU YA SERIKALI PALE BIFU ZINZPOKOTEZEA KWA RUGE BASI UHINGILIA KATI KUTAFUTA SULUHU KWA KWELI KUNAACHA MASWALI MENGI.
 
KWA MTAZAMO WA KIUNGWANA NI NI JAMBAO JEMA SANA WALAKINI YANGU KWA NINI IWE KWA RUGE TU AWALI WAZIRI NCHIMBI AKIWA NAIBU WA WIZARA YETU YA HABARI UTAMADUNI,VIJANA NA MICHEZO A AMEINGILIA KATI JAMBO LA RUGE NA MBILINYI (SUGU) NA SASA TUNASIKIA RUGE NA LADY J DEE
SERIKALI IMEINGILIA KATI MAONI WENGI MBONA KUMBUKA ASHA BARAKA WA TWANGA PEPETA NA MAMAA WA MASHUJAA HATA  TAFF NA BONGO BOVIE, VIKUNDI VYA TAARABU NI BAHADHI TU LAKINI WENGI WAPO WALIKUWA KWENYE MVUTANO MKALI LAKINI SERIKALI IKIWA KIMYA USHAURI WANGU HATUA HIYO NZURI SANA KULETA AMANI KWA WASANII LAKINI
IWE KWA WOTE BILA KUBAGUA WATATUE INAPOTEA MIGOGORO HATA YA KIMASLAI PIA KUONDOA DHANA KUWA RUGE ANAPENDELEWA SERIKALI MADHALA YAKE KWAHISIA HIZO NI KUBWA SANA,KUSIPO ZIBA UFA KUTAJENGA UKUTA TUCHUKUE HATUA SASA, MAANA SISI NDIO TUPO KARIBU NA WASANII MUDA MWINGI TUNAWAMBUSHA SERIKALI JUU YA UMUHIMU WATOA HUDUMA SAWA KWA WOTE BILAKUJALI UMAARUFU WA MSANII KWA KUANZISHA DAWATI LA  HUDUMA KWA WASANII ITASAIDIA SANA

MIMI

CHE MUNDUGWAO
MWENYEKITI- CHAMA CHA MUZIKI ASILI TANZANIA NA
MJUMBE WA BODI SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kusema kweli sio Ruge tu bali Clouds ina matatizo na wasanii wetu! kumbukeni walianzia na Mr Nice akaja Sugu na sasa ni Jay De.

    Mie naamini kuna kikubwa zaidi kimejificha nyuma ya pazia na sasa ni wakati wa wasanii KUANIKA ukweli wa Clouds.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2013

    Siamini kama rai hii imetolewa na mwanamuziki huyu mkongwe.Japokuwa kuna hoja ya msingi lakini cha kushangaza rai yenyewe haiko katika mpangilio unaoeleweka wala mtiririko mzuri.Kiswahili kilichotumika baadhi ya maneno yamekosewa lahaja zake.Nabaki najiuliza kama tunaambiwa kuwa msanii ni kioo cha jamii,inakuwaje huyo huyo msanii hata lugha yake ya asili inampa shida kuiandika,kibaya zaidi eti ni mwenyekiti wa chama cha muziki wa asili Tanzania!!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 11, 2013

    there you are, sijaelewa ilitaka kusema nini, labda ana kipaji cha miziki ya Asili lakini hakupata Shule ya kutosha. Kuesma kweli kama ni mwenyekiti wa taasisi, basi tuna matatizo ya uongozi. tusione aibu kujiendeleza

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2013

    Clouds ni taasisi Binafsi inayoongozwa kwa sheria za nchi yetu kama vyombo vingine vya habari
    Clouds pamoja na kuwa ni taasisi binafsi imeanzishwa kwa malengo ya kibiashara siyo kutoa huduma bila kuwa na faida
    Ugomvi wote huu unaotokea ni kwa jamii kukosa uelewa mpana katika mambo ya SOKO huria
    Wasanii wote ulimwenguni hutengenezwa na kukuzwa na vyombo vya habari
    Sasa ni uamuzi wa msanii kukubaliana na kufuata policy za hizo media ambazo zinamjenga na kumkuza huyo msanii
    Ukienda nje ya policy zao ukweli unakuwa umejiangusha mwenyewe
    HAPA CHA MUHIMU NI SERIKALI KUZIANGALIA HIZO POLICY ziko na mapungufu gani?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 11, 2013

    Umeongea ukweli mtupu Mwenyekiti wa music. Kumbe na wewe umeliona hilo! Ruge ndio huomba hao viongozi waingilie kati, nao wanakubali kwa kuogopa kuwa atatumia Radio kuwachafua. Hafai kabisa. Wanamuziki kumbe mna chombo chenu, fanyeni mikakati ya wote kukataa music wenu kupigwa na clouds halafu tuone hiyo jeuri ya Ruge! Ukipigwa tu music mnawafungulia mashtaka, kwa kufanya hivyo sijui nani atafungulia radio yao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...