Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais
Dkt.Mohamed Gharib Bilal na Waziri wa
Mambo ya Nje Bernard Membe wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi
wapya
waliopaishwa leo ikulu jijini Dar es Salaam.aliyesimama mbele kushoto no
Balozi
Liberata Mulamula anayekuwa Balozi Mpya wa Tanzania nchini
Marekani.Waliosimama
nyuma kutoka kushoto ni Balozi mpya wa Tanzania Uholanzi Wilson
Masilingi,Balozi
mpya wa Tanzania katika visiwa vya Commoro Chabaka Kilumanga,Mwakilishi
wa
kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Geneva Balozi Modest jonathan Mero
na
Balozi mpya wa Tanzania katika falme za Kiarabu(UAE)Mbarouk Nassor
Mbarouk.Kabla ya uteuzi Balozi Liberata Mulamula alikuwa msaidi wa Rais
Masuala ya kidiplomasia na aliwahi kuwa katibu mkuu wa nchi za Maziwa
Makuu.(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo ikulu jijini Dar es Salaam
amemwapisha Jaji Aloycius Mujuluzi kuwa
Mwenyekiti wa tume ya kurekebisha sheria
pamoja na mabalozi wanne watakaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi.Mabalozi
walioapishwa leo ni pamoja na Balozi mpya katika umoja wa Falme za kiarabu(UAE)
Mbarouk Nassor Mbarouk,Balozi mpya wa Tanzania nchini Uholanzi Wilson Masilingi,Balozi
mpya wa Tanzania katika visiwa vya Commoro Chabaka Kilumanga na Mwakilishi wa kudumu Tanzania Umoja wa mataifa Geneva Balozi
Modest Jonathan Mero.
Hongera sana Balozi Liberata Mulamula kwa kuapishwa kuwa Balozi wa Marekani. Tunaomba ukaendeleze kazi kama Balozi Mwanaidi Maajar, uwe Balozi wetu mzuri, wasilisha Tanzania wasilisha wanawake.
ReplyDelete