Meneja Matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho (wa pili kushoto) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo. Wengine pichani kutoka kushoto ni DJ John Dilinga (JD), Prodyuza Ally Baucha na Prodyuza Tudd Thomas.
Kutoka kushoto waliokaa ni msanii Stamina, DJ John Dilinga, Abdallah Mrisho, Ally Baucha na Tudd Thomas katika picha ya pamoja na washiriki wa The Vodacom Mic King waliosimama nyuma.
Wakali wa MIC wanaowania gari wakiwa katika pozi na gari hilo.
Wanahabari wakichukua baadhi ya matukio.
...Wakimsikiliza Abdallah Mrisho.
Hawa ndiyo wakali tisa wanaowania gari aina ya Toyota Funcargo (New Model).

Uongozi wa Dar Live Co. Ltd leo umetambulisha tamasha kubwa la kila mwaka la Usiku wa Hip Hop na fainali za kumtafuta Mkali wa Mic zijulikano kama 'The Vodacom Mic King' kwa wanahabari. Tamasha hili litafanyika Jumamosi hii, Mei 25, 2013 katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar. 

Jumla ya vijana tisa wenye vipaji watapanda stejini kuchuana na mshindi ataondoka na gari aina ya Toyota Funcargo (New Model) yenye thamani ya shilingi milioni 15. 

Mbali na zawadi ya gari, mshindi wa kwanza, pili na watatu, watapata fursa ya kurekodi wimbo mmoja chini ya Prodyuza mahiri nchini, Tudd Thomas, aliyerekodi wimbo maarufu wa Leka Dutigite wa Kigoma All Stars na nyingine nyingi. Majaji katika shindano hili ni mwandishi mkongwe wa habari za muziki na wasanii, Abdallah Mrisho, DJ John Dilinga (JD) na Prodyuza Ally Baucha.

Tamasha hilo litapambwa na burudani kutoka kwa wakali wa Hip Hop nchini ambao ni Fid Q, Joh Makini, Stamina, Kala Jeremiah, Nay wa Mitego pamoja na shoo kali kutoka kundi la Wakali Dancers. Katika usiku huo, zitatolewa tuzo kwa wasanii wa Hip Hop na kwa wimbo bora wa Hip Hop uliofanya vizuri mwaka 2012/13. 

Kutakuwa na Tuzo kwa Msanii Mkongwe Bora wa Hip Hop na Msanii Chipukizi Bora wa Hip Hop pamoja na Wimbo Bora wa Hip Hop.(PICHA NA MUSA MATEJA / GPL)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2013

    Ankali wakumbushe wandugu wa Hiphop kuhusu Mabingwa wa Mawe (Wakali wa Rap) hawa hapa chini wa miaka ya Kitambo kile cha 1989 !

    1.A Tribe Called Quest - Can I Kick It? ALBUM VERSION With Lyrics

    link:

    http://www.youtube.com/watch?v=ZrlJX7DzLhI

    2.THE BIG DADY KANE

    link:http://www.youtube.com/watch?v=NkNesld5ig0

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...