Wananchi wakifuatilia mzozo baina ya mfanyabiashara wa maji na mteja wake baada ya kubainika kwamba amemuuzia maji bandia.Mfanyabiashara huyo ametambulika kwa jina la Kagira Mhisho mwenye umri wa miaka 15 inaseemekana kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo kwa kutumia maji kutoka sokoni kariakoo kwa takribani miaka mitatu sasa.Ninvyema wananchi wakajihadhari na maji yanayouzwa njiani kwani baadhi ya wafanyabiashara wasiowaaminifu huokota chupa zilizokwisha tumika na kuzitumia.Ninashauri vyombo husika katika ukaguzi na kujali afya za walaji kuingilia kati ili kuepusha wananchi kupata maradhi mbalimbali.
Mfanyabiashara wa maji aliyetambulika kwa jina la Kigira Mhisho(15) akimwaga maji baada ya kubainika kuwa anauza maji bandia.(PICHA NA Frank Shija - MAELEZO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2013

    Ama kweli bongoland choka mbaya, hili njemba kabisa halafu mnasema ana miaka 15, haiwezekani huyu anakambilia huyu Thelathini huyu, sema kamekauka na kudumaa tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2013

    Inatisha na kusikitisha sana, anayeumia siku zote ni mwananchi wa hali ya chini au kawaida. kwani wenye uwezo hawanywi hayo maji. Mungu iponye TZ na watu wake.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2013

    Sasa jamnani maji bandia au maji yasiyofikia kiwango cha afya kwa ajili ya matumizi ya kunywa binaadamu!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 21, 2013

    Naona leo mjomba umeamua kutuchekesha. Yani huyo mdau ndio ana miaka 15!!! Au ulimaanisha 51!!?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 21, 2013

    Miaka kumi na tano (15) haiwezekani. Labda tuseme miaka 35.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 21, 2013

    Yote kwa yote Ama bandia ama yasiyoviwango huyo jamaa abinywe atawatajia mtandao wote_mjue hayuko mwenyewe na utakayemkuta nyuma ya hao ji njemba lkuuubwa! Aibu yetu wabongo!! Kajiseme tumiaka 15 anajua likibuma ataenda jela ya chekechea!! Chezea mbongowewe!! Mtakunywa refined shit!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 21, 2013

    Duh ndiyo mmeshtuka leo!! haloooo! mshakunywa maji ya kinyesi siku nyiiiingi jamaa kayapoooza matamuuuu Kudadeki Kinyesi mwe mnacho mwilini .... Chezea chingaz wewe! Rahisi ghali.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 21, 2013

    Tanzania kila kitu ni feki, maji, pads za wanawake za mwezini, madawa mengi, dawa za mbu, viungo vya kupikia na sasa mnayaona wenyewe maji FEKI jamani tuwe makini afya ya mtu si kitu cha kuchezea kabisa. sasa subirini mlipuko wa magonjwa maana maji feki inamaana hizo chupa watu wameshazitumia wakatupa huyu kijana na wenzake wanazitumia tena kuuzia watu maji machafu. magonjwa.com

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 21, 2013

    Sasa kumwagwa kwa hayo maji ndio ufumbuzi wa tatizo?? watanzania wanatia huruma kweli masikini yaani hata hawajui wafanye nini inapotokea hali zinazofanana na tukio kama hili,Mimi nilidhani watamfikisha kituo cha usalama kisha waanze mkakati wa kuwatafuta wengine ikiwemo na viwanda yanapotengenezwa hatimae kumaliza tatizo,Yaleyale kila mtu yuko bize na shughuri zake wala hawastushi na matukio kama haya,nina hakika kesho muujazi atabadili nguo na mtaa maji ni yaleyale.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 22, 2013

    kwakweli kuna ule msemo unaosema kila mtu ana kula kulingana na urefu wa kamba yake. Mimi napenda kusema kuwa, kaka =Michuzi ungeanza kwanza na kuwafichua mafisadi na wachukukuliwe hatua za kisheria na ndipo uanze na wale walala hoi. Maana hata yeye yupo katika kutafuta riski yake. Ila, yote ni kwamba Mwenyezi Mungu anatulinda siku zote, maana ni vingi tunakula tukiwa nje ya majumbani mwetu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 22, 2013

    KITUO CHA USALAMA?JAMAA ANA MIAKA 15 BADO NI MTOTO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...