THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MTANGAZAJI JOYCE KIRIA AMTAFUTA MUMEWE KWA MABANGO

1a
Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake ndani ya Kituo cha Televisheni cha EATV,Joyce Kiria akiwa amewashikilia watoto wake Lingatone Kileo (kulia) na Lincorn wakati alipozungumza na waandishi wa habari nje ya Jengo la Idara ya Habari Maelezo iliopo katika mtaa wa Samora,jijini Dar huku akipaza sauti kuomba msaada kwa Rais Jakaya Kikwete na watanzania kwa ujumla ili kusaidiwa na kujua aliko mume wake,Bw. Henry Kileo ambaye inadaiwa kuwa anashikiriwa na Jeshi la Polisi, Joyce Kiria amesema mpaka sasa hajaambiwa kama mume wake yuko wapi hivyo hata kama ana makosa anaomba afahamishwe kwani hajui kinachoendelea mpaka sasa.
3
Joyce Kiria akifafanua mambo mbalimbali mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo huku akiwa amewabeba watoto wake na ndugu zake wengine wakiwa na mambongo yenye ujumbe mbalimbali.
4

Joyce Kiria akendelea kujibu maswali kadhaa ya wanahabari wakati akizungumza nao leo jijini dar es salaam.Picha kwa hisani ya FullshangweBlog.
Advera Senso Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania
--
 Inasikitisha kuona kwamba huyu mama Joyce Kiria anaingilia mambo ya kisheria na kutaka kupotosha jamii kwamba hajui mume wake yuko wapi pia nadhani analenga kuichochea jamii kwamba aliyetuhumiwa kutenda uhalifu akikamatwa familia yake iandamane, tendo ambalo pia ni kosa la jinai. Aidha anatakiwa kuheshimu haki za watoto na kuacha kuwatumia katika kinga ya kutetea watu wanaotenda uhalifu 

Imetolewa na
 Advera Senso 
Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini TanzaniaKuna Maoni 24 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Walipata wapi kibali cha kuandamana hawa???wapiga mabomu wapi???pinda nae hahhhahahahha haya sasa.

 2. Anonymous Anasema:

  Bongo full usanii, ina maani hujui mume wako yuko wapi??acha kutupiga kiini macho aisee, tayari mshafanya ufisadi halafu mnaizuga jamii.

  hiki ni kiini macho , Polisi fanyeni kazi yenu bana

 3. Anonymous Anasema:

  LOL!! hahahaha amuulize bwana wake anafanya biashara gani jamani? maana mume hawezi chukuliwa na mapolice hivi hivi bila sababu maalimu jamani. Haya nayo Majanga. Yetu macho na masikio.

 4. Anonymous Anasema:

  Acha basi kudandia treni, mumewe alikamatwa na polisi. Alipopeleka chakula central police hakumkuta na majibu aliyopewa na polisi ni kuwa hajulikani alipo. Wakili wake pia hakupewa taarifa kua mteja wake ameachiwa huru au la!
  Kwa jinsi mambo yalivyo nchini na polisi wasioaminika mlitaka afanyeje? Kwanza ni mmoja kati ya wanawake jasiri japo wengi watamuona kama chizi. Ila ni haki yake kujua mumewe yukoapi. Polisi hamuaminiki na mtazidikutoaminika

 5. Anonymous Anasema:

  Pole sana mama! inaumiza sana ni mbaya sana hata siku moja ikipita bila kujua mwenzi wako yuko wapi hata ukijua eneo alipo je ni kwa sababu gani? huwezi kulala kwa stress. hasa mkiwa mna familia ambayo inawahitaji kwa leo na kesho. Mpaka mtu anaamua kusimama hivyo ni ameshahangaika sana jamani. Wahusika kwa taratibu zenu za kikazi msaidieni.ni binadamu huyo ana hisia kama sisi basi tujali hisia za wenzetu na haki ya kupata habari.

 6. Anonymous Anasema:

  Huyu mm sio mzima! Analeta ujinga mbele ya jamii ili ainekane mumewe hana makosa? Henry kileo alitoa taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba ameitwa polisi kuhojiwa na amemjulisha wakili wake, je,ni kweli hajamwambia mkewe? Ina maana wakili wake ni muhimu kuliko mkewe na watoto! Aache kujishaua hapa! Wauaji wakubwa.

 7. Anonymous Anasema:

  Asitake sympathy ya jamii huyu. Mumewe ana wakili na wakili yuko bize facebook kupost yanayojiri kuhusu mumewe...amuulize wakili mumewe yuko wapi. Wakati akisimama na mabango wakili wa mumewe alikuwa Tabora na huyo mume mahakamani. Ndoa ni msalaba mama anza kuubeba kwa furaha usituhusishe. Juzzi kwenye kipindi chako ulimponda mume wa zamani...haya sasa raha ya mume mpya huyo. Mtu aliyepotelewa na mume anamuda wa kuchana nywele? Hahahhaa

 8. Anonymous Anasema:

  dada Joyce kuna ngazi za kufatilia za kudai taarifa ya mumeo alipo haya maandamano ya bila kibali na hizi serikali zetu za joto hasira watakubeba upelekwe segerea mjikute wote mnaacha watoto wanahangaika na wanandungu nakushauri dai haki yako kwa kufata sheria ukivunja sheria na wewe utakua umewapa sababu ya kukuchukua na wewe pole sana

 9. Anonymous Anasema:

  nadhani mama huyu hamtetei mumewe kuwa hana kosa bali anataka kujua amepelekwa wapi kwani ni mtuhumiwa tu.

 10. Anonymous Anasema:

  Dada, ukipotelewa na mtu wako unakwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi kilicho karibu nawe, then unawaachia Polisi kazi ya kumsaka. Kwa hili ulilolifanya umejiabisha sana as if hujui Kileo ni nani hapa mjini.

 11. Anonymous Anasema:

  MUME WAKO YUPO LUPANGO !

  Habari ndiyo hiyo JOYCE KIRIA mumweo amevunja Sheria za nchi kwa Uhalifu hivyo amewekwa Mbaroni!

 12. Anonymous Anasema:

  Police kumkomesha huyu mama tuambieni kafanya nini huyo kaka.

 13. Anonymous Anasema:

  Mnaodhihaki huyo mama acheni zenu hizo. Kuna siku yatawakuta na yatakuwa machungu kuliko yaliyompata huyo mama.

 14. zamsquared Anasema:

  pole sn mama

 15. Anonymous Anasema:

  wewe mtoa maoni hapo juu unafahamu lugha au ni mwanafunzi wa darasa la pili? hivi ndio maana wanafunzi wanafeli mitihani kwa kushindwa kuwa na ufahamu wa kusoma.

  Kuitwa polisi kuhujiwa haina maana ya kuwa unawekwa kuzuizini, na hata baada ya mahojiano na polisi wakiamua kukuweka kuzuizini familia yako wakifuatilia wanajua ulipo.

  Kileo amesema ameitwa polisi kuhojiwa na baada ya hapo ndio hajulikani alipo, polisi wanashindwa hata kumjulisha wakili wake mteja wake yuko wapi sasa utasemaje kuwa huyu mama sio mzima kwa kutaka kujua alipo mumewe?

  Amkeni watanzania, tutokane na imani zile za kikoloni za kuwa polisi hafanyi kosa wala haulizwi maauzi anayoyafanya.

 16. Anonymous Anasema:

  Tatizo CHADEMA wamezoeleka ndio chanzo cha vurugu nchini hivyo hata kama ni kweli anaonewa ni ngumu sana kuamini.

 17. Anonymous Anasema:

  Tafadhali advera , hebu fikiria kama angekuwa mmeo amekamatwa then hujui yuko wapi kwa muda kadhaa.

  Nakushangaa unaposema anaichichea jamii. Hapa yeye anaogopa. Mara ngapi tumesikia watuhumiwa ( kama ni mtuhumiwa) wanafia kwenye vituo vya polisi?

  Inawezekana hata wakili wake asipewe taarifa aliko mteja wake. Si haki za raia wa TZ ziko mikononi mwa polisi?Mzee Pinda alishahalalisha kipigo kwa wananchi.

  Polisi mmepewa baraka ya kupiga . Na huyu jamaa inawezekana akapigwa mpaka akafa . Hebu mjulisheni mmewe yuko wapi Advera acha kummbania menzio.

 18. Anonymous Anasema:

  Jamani acheni kumkejeli huyu mama bila kuelewa story yake...hao polisi walisema hawajui mme wake alipo,sasa yeye afanyaje?kwani hata kama mme wake huyo ana makosa na kashikiliwa na polisi si inapasa ijulikane ni kituo gani yupo? Au siku hizi watu wakishikiliwa na polisi ni kwa siri?

 19. Anonymous Anasema:

  Ingekuwa rahisi sana kueleza kama anashikiliwa (hata kwa kusema anashikiliwa na polisi kwa mahojiano) bila mlolongo mzima wa maneno mengi yasiyo na tamati

 20. Mdau Uk Anasema:

  SIJAJUA KM KUNA BAADHI YA WATANZANIA NI WAJINGA HIVI HAPO JUU MMESHAELEWESHWA WEEE BADO MNAJIFANYA HAMUELEWI...MBONA BAADA YA HAYA WAMEMUONYESHA MUME WAKE...POLE JOYCE...YATAKWISHA TU..

 21. Anonymous Anasema:

  TUKUMBUKE:

  Sio vema kuchukulia kuwa moja kwa moja ameonewa kwa kuwa suala la Majukumu ya Kifamilia na kutenda Uhalifu ni Usiku na Mchana.

  Kama utaitwa BABA au MUME halafu ukatenda Uhalifu usifikiri KUWA MOJA YA HIZO KOFIA ZAKO HAPO JUU ZA KUITWA BABA AMA MUME ZITAIPINDISHA SHERIA KUKUGANDAMIZA.

  NI LAZIMA ITATOA USHIRIKIANO UTAWEKWA MBARONI, UTAFIKISHWA MBELE YA SHERIA KWENYE MAHAKAMA UTAHUKUMIWA NA BAADA YA HUKUMU HAPO NDIO MAHAKAMA NA WAZEE WA BARAZA WATAKUWA NA JUKUMU LA KUKUFIKIRIA KUPUNGUZIWA ADHABU KWA UZITO WA HUO 'UBABA' NA 'UMUME'!

  PANA NCHI DUNIANI MLISIKIA MTU AKIWA BABA AMA MUME NDIO AFANYE UHALIFU NA KUKINGIWA KIFUA?

 22. Anonymous Anasema:

  Inapokuwa Sheria na Taratibu za Uendeshaji wa Makosa, hata kama Dunia ipo kichwani kwako kwa majukumu, haiwezi kuwa sababu ni lazima Mgandamizo wa Nyundo ya Mkono wa Sheria itaelekezwa hapo hapo juu ya hiyo Dunia uliyoibeba Kichwani kwako!

 23. Anonymous Anasema:

  Advera,huyu mama anajua kama mumewe yuko polisi,lakini alivyompelekea mumewe chakula,hakumkuta,na hadi siku hiyo hawakumwambia wamempeleka wapi,na wala wakili wake hajaambiwa kuwa kapelekwa wapi Kileo,

  Ni haki na mtu wa karibu wa mtuhumiwa ajulishwe mtuhumiwa kapelekwa wapi,kama segerea,au wapi wapi,lakini si kumficha,

  GOD BLESS TANZANIA NA WATU WAKE

 24. Anonymous Anasema:

  Mbona akiwa studio habebi watoto?

  Hayo mabango na mkusanyiko umetayarishwa lini na nani?

  Hahahaha, ati unamtafuta mumeo...haya nenda Igunga kule alikommwagia tindikali mume wa mwanamke mwenzio na baba wa watoto kama wako