JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

NAFASI ZA AJIRA ZA KADA ZA AFYA KWA MWAKA 2012/2013

Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, anapenda kuwaarifu Wataalamu wa Kada za Afya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi kutokana na maombi ya kazi waliyowasilisha kwake kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Watalamu wote wanatakiwa kuripoti katika vituo walivyopangiwa kabla ya tarehe 30 Juni, 2013. Baada ya muda huo kumalizika waajiri wanatakiwa kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili wale ambao hawajaripoti nafasi zao ziweze kujazwa.

Aidha, Waajiri wote wanakumbushwa kukagua vyeti halisi (Original) vya kidato cha nne na kidato cha Sita pamoja na vyeti vya taaluma kabla ya kuwaajiri wataalamu hawa wa kada za afya.

Orodha ya majina ya Wataalamu waliopangiwa kazi na vituo walivyopangiwa inapatikana kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz. Wizara haitatoa barua za kupangiwa vituo vya kazi kama ilivyokuwa hapo awali.

Nawapongeza kwa kupata nafasi hii ya kutumia utaalamu wenu katika kuwahudumia wananchi, na ninawatakieni kazi njema na utumishi uliotukuka.

20 Juni, 2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...