Kikao cha Viongozi wa Tawi la Chadema Washington DC, Marekani, tarehe 27 July 2013 kimemteua Ndugu Kalley Ammy Pandukizi kuwa Mwenyekiti wa Tawi kuchukua nafasi ya Ndugu Cosmas Wambura.

 Awali Ndugu Kalley Pandukizi alikuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tawi la Chadema DMV linalobeba majimbo matatu ya Washington DC, Maryland na Virginia. Baadae alikuwa Afisa wa Habari wa Tawi na nafasi yake kuchukuliwa na Cosmas Wambura. 

Viongozi wengine na nafasi  zao ni Katibu wa Tawi niLibearatus Mwang’ombe aliyekuwa  katibu wa kwanza wa Tawi, aliyechukua nafasi ya Isidory Lyamuya. 

Katibu Mwenezi ni Ndugu Hussein Kauzela na Mweka hazina ni Ndugu Ludigo Mhagama. Mwenyekiti wa Baraza la wanawake ni Ndugu Baybe Mgaza na Katibu wa Baraza la wanawake ni Mariam Khamis. Nafasi nyingine ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Ndugu Amri Maliyatabu na katibu wa baraza la vijana ni Ndugu Stephen Msungu.

 Nafasi nyingine ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee ni Amos Cherehani na Katibu wa baraza la wazee ni Elias Mshana. Nafasi ya Mwisho ni ya Baraza la Washauri linaloongozwa na Prof Nicolas Boaz na Emmanuel Muganda.

Akizungumza baada ya Uteuzi huo Mwenyekiti wa Chadema Washington DC Ndugu Kalley, Amewashukuru Viongozi wote kwa kumwamini na kumpa nafasi hiyo kwa mara ya pili na kuwaahidi kufanya mambo makubwa ikiwemo kurudisha uhai wa Tawi na kuwaunganisha wanachama kuwa wamoja. 

Pia ameahidi kushirikiana na Jumuia nyingine ikiwemo Jumuia ya Watanzania DMV, Ofisi ya Ubalozi Wa Tanzania Marekani, Jumuia ya Waislam waishio Washington DC (TAMKO) na Uongozi wa CCM DMV ili kujenga Tanzania Moja yenye mshikamano.

Pia Ndugu Kalley amesema baada ya kurudi kwenye nafasi hiyo kipaumbele cha kwanza kitakuwa kuvalia njuga mambo makuu mawili ambayo ni Suala la mchakato wa Katiba unaoendelea ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapata Katiba nzuri iliyoridhiwa na Watanzania wote bila kuingiliwa na mtu yeyote kwa nia mbaya. 

Pili amesema atavalia njuga suala la upatikanaji wa Tume huru ya Uchaguzi ili Uchaguzi Ujao wa Mwaka 2015 uwe huru na Haki.

Aidha Katika mkutano huo Ndugu Kalley ameelezea kusikitishwa sana na vitendo vya ukiukwaji wa Sheria vinavyofanywa na Jeshi la Polisi kwa kuwabambikizia kesi raia wasio na hatia na hata matukio ya mauaji wanayotuhumiwa baadhi ya Askari Polisi. 

Ndugu Kalley amesema atapambana vikali kuhakikisha matukio hayo ya ukiukwaji wa haki za raia yanayofanywa na baadhi ya askari Polisi yanakomeshwa, kwani hakuna sheria inayoruhusu askari Polisi kujichukulia sheria mkononi wakati Mahakama ndizo zilizopewa Mamlaka hiyo.

Tawi la Chadema Washington DC lilianzishwa rasmi tarehe 26 Aprili 2012 chini ya usimamizi wa Mbunge wa viti maalum Mh Leticia Nyerere na Kufunguliwa rasmi tarehe 27 Mei 2012 na Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu katibu mkuu wa Chadema Mh Zitto Kabwe. 

Sherehe hizo za Ufunguzi ziliudhuriwa Pia na Mbunge wa Iringa mjini Mh Peter Msigwa, Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari, Mbunge wa Viti Maalum Kwimba Mh Leticia Nyerere na Mbunge wa Viti maalum Kutoka Zanzibar Mh Mariam Msabaha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. CDM kwenu ni kuteuana tu hata kwenye nafasi zinazohitaji demokrasia. haya tuambieni mnamteua nani 2015

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...