Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani umemfanyia hafla fupi ya kumtambulisha Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwa kwa Whe. Mabalozi wa nchi jirani na nchi marafiki wa Tanzania wakiwemo viongozi wa jumuiya mbalimbali za Watanzania DMV. Kwenye picha Kaimu Balozi na Mkuu wa Utawala na Fedha Mama Lily Munanka (kati) akimkaribisha Mhe. Balozi Liberata Mulamula mara tu alipowasili Ubalozini hapo akiambatana na familia yake, kulia ni Charles Gray ambaye ni Balozi wa hiari anayeitangaza Tanzania nchini Marekani na anayeishi Pennsylvania kwenye mji uitwao Bala Cynwyd.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Charles Gray.
Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa.
Mhe. Liberata Mulamula akiongea jambo na Mhe. Edward Lowassa.
 Kaimu Balozi na Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka akiongea machache yakiwemo kuwakaribisha Whe. Mabalozi na Viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania DMV kwenye Hafla hiyo fupi na baadae kumkaribisha Mhe. Balozi Liberata Mulamula kuongea nao.
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea machache yakiwemo kuwashukuru Maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi kwa kuandaa Hafla hiyo fupi ya kumtambulisha kwa Whe. Mabalozi wa nchi jirani na nchi marafiki wa Tanzania na Viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania DMV wakiwemo wanahabari wa DMV pia alielezea kwamba leo Alhamisi July 18, 2013 alipeleka hati yake ya utambulisho kwa Rais Barack Obama na anafuraha kukutana nao hapo Ubalozini na hii isiwe mwisho wanakaribishwa muda wote wajisikie wapo nyumbani.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Afisa Mindi Kasiga ili aongoze kuimba wimbo wa Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote. Mindi Kasiga ndiye aliyekua mshereheshaji wa Hafla hiyo.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akitambulisha familia yake kutoka kushoto ni mwanaeTanya, Alvin na Mumewe Bwn. George Mulamula.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifanya tosi.
Whe. Mabalozi, Viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania DMV, wageni waalikwa wakitosi pamoja na Mhe. Balozi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2013

    Karibu balozi, mimi mdau wa dmv nafarijika nikiona wamama wakiwajibika ipasavyo, nataka pia nimsifie huyu kaimu, Mama Munanka, kweli huyu ni imara, chapa kazi, na iron lady, hazina kubwa ya watz, Mheshimiwa Rais aombwe ampe full ambassador kabisa, au wadau wa dmv naongopa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...