THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue atembelea Banda la PPF kwenye Maonyesho ya Sabasaba jijini Dar

Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio akimpa maelezo Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo alipotembelea katika banda la PPF katika maonyesho ya 37 ya kimataifa ya biashara katika viwanja vya Sabasaba.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi Joyce Mapunjo, pembeni yake ni Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade Bi Jacqueline Maleko.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Erio akimsindikiza Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue na ujumbe wake mara baada ya kutembelea banda la PPF.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira Mh. Eric Shitindi akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa PPF Bwana Thomas Chissanga. Katikati ni Meneja Uhusiano na Masoko wa PPF Bi Lulu Mengele.
Meneja Uratibu wa Ofisi za Kanda za PPF Bwana Mbaruku Magawa akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira Mh. Eric Shitindi alipotembelea banda la PPF. Kulia ni Meneja Uhusiano na Masoko Bi Lulu Mengele.
Afisa wa Sheria wa PPF Bi Nyambilila Ndoboka akimpa maelezo Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira Mh. Eric Shitindi. Pembeni ni Mameneja wa PPF, Bwana Mbaruku Magawa na Bi Lulu Mengele.