Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk.Mohamed Gharib Bilal akifungua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi kwa ujenzi wa jengo la Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Shule ya Msingi Kisiwandui mjini Zanzibar juzi. Kushoto kwake ni Mbunge wa Kikwajuni, Hamadi Yussuf Masauni. Vodacom Foundation imesaidia saruji yenye thamani ya Sh.Milioni 10 kufanikisha ujenzi huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano,, Dk Mohamed Gharib Bilal akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Shule ya Msingi Kisiwandui katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, mjini Zanzibar juzi. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Kikwajuni Hamadi Yussuf Masauni na Meneja wa Vodacom Hassan Saleh.
Mbunge wa Kikwajuni, Hamadi Yussuf Masauni akizungumza mara baada ya Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal (wa pili kulia) kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Shule ya Msingi ya Kisiwandui, mjini Zanzibar juzi.
Mwenyekiti wa Vodacom Foundation, Hassan Saleh (kulia) akikabidhi moja ya kompyuta kwa Makamu wa Rais wa Tanzania Dk.Mohamed Gharib Bilal kwa ajili ya Shule ya Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Chwaka hafla iliyofanyika wakati wa uzinduzi wa kituo kama hicho katika Shule ya Msingi Kisiwandui Mjini Zanzibar juzi.
Makamu wa Rais, Mohamed Gharib Bilal (kulia), akiagana na Mbunge wa Kikwauni, Hamadi Yussuf Masauni mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Kituo cha Habari na Mawasiliano katika Shule ya Msingi ya Kisiwandui, mjini Zanzibar juzi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...