Dj Luke akiambatana na mgeni wake Rais Mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi kuelekea ukumbini kulikofanyika Tamasha la Utamaduni wa kiswahili na sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo Jumamosi July 6, 2013 na kuwa tamasha la kihistoria lililohudhuriwa na Watanzania wakiwemo wadau wanaozungumuza Kiswahili wapatao 600 kutoka kila kona hapa Marekani, Ulaya na Tanzania.
Kutoka kushoto ni Dj Luke, Mhe, Ali Hassan Mwinyi, Mhe. Ramadhan Muombwa Mwinyi, Mama Lily Munanka, Idd Sandaly na Baraka Daudi katika picha ya pamoja wakati wakiingia ukumbini.
Watoto wa darasa la Kiswahili DMV wakiimba wimbo wa Taifa.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi akiongea machache kabla ya kumkaribisha Dj Luke.
Dj Luke akisoma hotuba yake kabla ya kumkaribisha Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka.
Kaimu Balozi Mama Lily Munanka akishukuru kamati ya maandalizi na kumkaribisha mgeni rasmi Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akihutubia mamia ya Watanzania waliofika kwenye Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili na sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na kulifungua rasmi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York, Bwn. Haji akisoma shairi alilotunga maalum kwa ajili ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la Utamaduni wa kiswahili Marekani.
Shilole na Masanja mkandamizaji wakikandamiza na kugaragaza kwenye Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili na miaka 3 ya sherehe ya Vijimambo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2013

    Ilitakiwa kumwambia Masanja avue hiyo shati coz it is disrespectful to our Nation and Flag

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2013

    Mbona mama Siti Mwinyi umemruka kwenye ile picha ya kwanza?

    Au hukumfahamu?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2013

    Kwani shati lina nini? Mbona Masanja kapendeza sana na shati lake? @Mdau mtoa mada wa kwanza kabisa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...