Sehemu ya zawadi walizokabidhiwa washindi ambapo ilikuwa ni ng'ombe mmoja na mbuzi watatu.
 Waandaji na wasimamizi wa mashindano hayo viongozi wa KDFA wakipeana majukumu wakati wa fainali.
 mashabiki na wachezaji wa Mtonga FC wakishangilia ushindi
  mabingwa wapya wa mashindano ya Gambo Cup Mtonga FC baada ya kutawazwa mabingwa.
 baadhi ya wafanyakazi wa NMB tawi la Korogwe wakifuatilia utoaji wa zawadi.
 Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe Chiku Galawa akizungumza kabla ya kutoa zawadi.
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akimpongeza mchezaji bora wa mashindano hayo aliyepata zawadi ya mpira.


Picha na Habari na
 Mashaka Mhando, Korogwe
MASHINDANO yaliyodumu kwa miezi mitano ya kugombea kombe la Mkuu wa wilya ya Korogwe Mrisho Gambo, 'Gambo Cup', yamefikia tamati kwa timu ya soka ya Mtonga FC, kutwaa kombe, Ng'ombe, jezi na mpira walizokabidhiwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni (mstaafu) Chiku Gallawa.
Fainali hiyo ilizozikutanisha timu zenye historia tofauti huku Mtonga timu iliyoundwa na vijana wadogo ilionekana kabla ya mchezo kuanza itafungwa na wapinzania wao Manundu United ambayo tayari imekuwa na udhoefu mkubwa hasa kutokana na kushiriki mashimndano makubwa yakiwemo Ligi ya Taifa ngazi ya Mkoa wa Tanga.
Lakini, vijana hao waliuanza mchezo huo mithiri ya nyati aliyejeruhiwa kisha kumsaka mbaya wake pale alipopata bao la kwanza lililofungwa na Selemani Msagama aliyeihadaa ngome ya Manundu kisha kuutumbukiza mpira kimiani kuandikia timu yake bao la kwanza dakika ya 29.
Manundu timu yenye mashabiki lukuki iliyoingia uwanjani kwa mbwembwe zote kuwagonga majirazi zao hao, walisawazisha bao hilo dakika ya 35 baada ya mchezaji wao mmoja kuwatoka mabeki wa Mtonga na kumimina majalo yaliyoungwanishwa vizuri kwa kichwa na Abdallah Shauri.
Mtonga ambao baada ya kunywakua kombe hilo, wameaahidi kujisajili mwakani ili washiriki Ligi ngazi ya wilaya, iliandika bao lake la ushindi dakika ya 43 lililopachikwa kimiani na Charles Daffa ambaye kabla ya kufunga bao hilo alimvika kanzu beki wa Manundu kisha kufunga kwa shuti kali.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, katibu wa Cha Soka wilayani Korogwe (KDFA) Zaina Hassain, walimshukuru Mkuu wa wilaya kwa kuanzisha mashindano hayo ambayo yame;leta changamoto mpya kwa vijana wilayani humo na kuibua vipaji kutokana na timu 84 kushiriki mashindano hayo katika ngazi ya kata.

Mkuu wa mkoa alisema kwamba mshindano hayo yamemfanya afikirie kuanzisha mashindano yake akishindanisha wilaya zote lengo likiwa ni kuibua vipaji na kuwafanya vifanya waweze kucheza wakiamini kwamba mpira wa soka miaka ya hivi karibuni ni ajira mojawapo kwa vijana.
"KWA kweli nimependa jinsi mlivyojipanga hadi mkafanikisha fainali hii nakupongeza Mkuu wa wilaya (Gambo) kwa kuandaa michuano hii...Nami nitaanzisha ya kwangu nitayaita Gallawa Cup, najua mtanisaidia kwa vile mmepata udhoefu na mna halmshauri mbili hapa," alisema Mkuu huyo wa mkoa.
Mashindano ambayo yamedhaminiwa na benki ya National Micro-Finance (NMB) waliotoa zawadi za vifaa pamoja na kombe, yalitia fora kwa kujaza watu wengi kwenye fainali hiyo ambayo msemaji mmoja alisema kwamba idadi ya watu walijitokeza kushuhudia fainali hiyo haijawahi kutokea kwenye uwanja wa Chuo Cha Ualimu Korogwe. Mashindano hayo yamefanyika kwa gharama ya shilingi milioni 21.
Mshindi wa kwanza alipata Kombe, Ng'ombe, Jezi seti moja na mpira, wakati mshindi wa pili alipata mbuzi wawili, jezi na mpira huku mshindi wa tatu akipata mbuzi mmoja, jezi na mpira, sambasamba na waamuzi kupewa zawadi ya fulani, firimbi huku viongozi wa KDFA wakipewa zawadi ya nyavu kwa ajili ya magoli.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...