kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars' kilichokipiga leo na timu ya taifa ya Uganda.
kikosi cha timu ya taifa ya Uganda 'Uganda Cranes'
Mchezaji wa timu ya Taifa "Taifa Stars" Aggrey Morris (katikati) akiwania mpira huku akizongwa na mabeki wa Uganda Cranes wakati wa mchezo wao wa Marudiano uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala Uganda.hadi mwisho wa Mchezo Taifa ilichapwa mabao 3-1
Amri Kiemba akiambaa na mpira huku akizongwa na beki wa Uganda Cranes, Nicolas Kadada.
David Luhende akiambaa na mpira huku beki wa Uganda Cranes Said Kyeyune akijaiandaa kumkabili.
Mrisho Ngasa akiwania mpira na Nicolas Kadada wa Uganda Cranes.
Washabiki wa Taifa Stars wakishangilia goli la kusawazisha.

Tanzania (Taifa Stars) imeshindwa kufuzu Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) kwa mara ya pili mfululizo baada ya leo (Julai 27 mwaka huu) kufungwa mabao 3-1 na Uganda Cranes, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 4-1.

Stars ambayo ilicheza fainali za kwanza zilizofanyika Ivory Coast mwaka 2009 ilimaliza kipindi cha kwanza katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Kampala ikiwa sare ya bao 1-1.

Wenyeji ndiyo walioanza kufunga bao dakika ya saba katika mechi hiyo iliyochezeshwa na Kanoso Abdoul Ohabee kutoka Madagascar. Frank Kalanda alifunga bao hilo akimalizia mpira uliopigwa ndani ya eneo la hatari la Tanzania.

Bao hilo halikuonekana kuichangaza Taifa Stars, kwani ilitulia na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 18 mfungaji akiwa Amri Kiemba kutokana na pasi nzuri ya Mrisho Ngasa kwenye kona ya eneo la mita 18.

Dakika ya 32 nusura Taifa Stars ipate bao, lakini mkwaju maridadi wa Mrisho Ngasa ambao tayari ulikuwa umempira kipa HAmza Muwonge uligonga mwamba kabla ya kuokolewa na mabeki wa Uganda Cranes.

Mabao mengine ya Uganda Cranes yalifungwa dakika ya 48 kupitia kwa Brian Majwega na lingine dakika ya 63 mfungaji akiwa tenda Kalanda kutokana na makosa ya Salum Abubakar kupokonywa mpira wakati akiwa katika nafasi nzuri ya kutoa pasi kwa mwenzake.

Kocha Kim Poulsen alifanya mabadiliko dakika ya 43 kwa kumuingiza Simon Msuva badala ya Frank Domayo aliyeumia, na dakika ya 78 akawaingiza kwa mpigo Haruni Chanongo na Vincent Barnabas badala ya David Luhende na John Bocco. Hata hivyo mabadiliko hayo hayakubadili matokeo ya mchezo.

Kikosi cha Stars kilipangwa hivi; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, David Luhende/Vincent Barnabas, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Frank Domayo/Simon Msuva, Salum Abubakar, John Bocco/Haruni Chanongo, Amri Kiemba na Mrisho Ngasa.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itarejea nyumbani kesho (Julai 28 mwaka huu) saa 4 usiku kwa ndege ya PrecisionAir.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2013

    wako wapi akina Thomas Ulimwengu na Samatta

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2013

    Hivi tutatia aibu kwenye football mpaka lini? Mm mipango yangu hii hapa,1 tuwaombe radhi FIFA ili tusijihusishe kwenye mambo ya football ndani ya miaka 5 ili tujipange kuanzia vijijini mpaka matown,2 hao wazamini ndani ya hiyo miaka 5 kazi yao iwe kujenga vituo vya kisasa vya kukuzia vipaji vya watoto wetu na viwe vingi kama hizo shule za KATA nchi nzima,3 hiyo mipesa anayolipwa huyo KOCHA zipelekwe huko kwenye vituo,4 kila mtz nilazima achangie kiasi furani kila mwezi hasahasa matajiri ili kuvitunza hivo vituo,5 serikali ilete walimu toka nchi mbali mbali kama vile SPANISH,BRAZIL,UINGEREZA,mm nasema hivi kabra ya hiyo miaka 5 tutaona umuhimu wa hivyo VITUO...ni mm mdau ninae umizwa na TEAM YETU YA TAIFA STARS.ifike mwisho tuseme inatosha sasa tuna taka MABADILIKO YA UKWELI,mungu ibariki TANZANIA.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2013

    Poleni TAIFA STARS mmetuwakilisha vizuri mchezo ulikuwa wa kiwango kizuri mmejituma kwa moyo na juhudi zote, sitosema bahati haikuwa yetu hatukwenda Uganda kubahatisha tumekwenda kuwashinda. Uganda Cranes ni timu mzuri wamecheza pamoja kwa kuelewana muda mrefu,tujipe moyo wa kujipanga upya, kama kawaida kipindi cha pili dakika za mwisho bado tatizo kubwa la Taifa Stars kutokuwa na uwezo wa nguvu za kumalizia mchezo,mazoezi ya aina gani yatumike kuwaongezea pumzi za kumalizia kipindi cha pili kuwepo na mabadiliko ya mchezo.
    mikidadi-denmark

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 28, 2013

    Wafanye nini hao kina samatta? Mimi narudia kauli yangu ileile ikiwa wachezaji hawalipwi vizuri basi siku zote hatufiki popote!!! Pesa ndio kila kitu bwana!!! sio pesa ya chai walipwe pesa nzuri uwone kama hatutofika mbali!! Mchezaji kima cha chini cha mshahara ate list milion 5 basi nakwambieni uhakika tutafika mbali. Chezea fedhaa!!! Weweee!!!!

    ReplyDelete
  5. Hakuna cha kulipwa vizuri wala nini!!! Hao watoto wanajidekeza! Wenzao walifanikiwa kucheza CHAN 2009 walikuwa wanalipwa kidogo kuliko wao!! Sasa mi napendekeza wapokewe kwa bakora wote na timu ivunjwe!! TUMECHOKAA!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 28, 2013

    sasa hivi mbona bongo twafungwa na kila nchi?..inasikitisha sana...

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 28, 2013

    wachezaji wetu hasa washambuliaji sio wabunifu hata kidogo.kwanza hawakai na mpira na kuwashosha viungo na mabeki mda wote.kocha atafute wachezaji wabunifu wanao weza kutengeneza nafasi na kufunga.pia wenye uwezo wa kufisha mpira sio kupoteza kirahisi.hapo tutakuwa na timu imara.mpira wanacheza ila bila mipango.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 28, 2013

    Tanzania imekuwa ni taifa la under-performers. Kuna article ilitoka kwenye gazeti moja, sikumbuki mwandishi wake, inasema tunajenga taifa la wajinga. Ubovu wa utekelezaji unaonekana wazi kwenye kila ngazi ya uongozi kuanzia juu hadi ngazi za chini. Angalia wizi wa mali za uma ulivyoshamiri, mabomu yanalipuka makanisani na kwenye mikutano ya hadhara na wananchi hawaambiwi kinachoendelea ni nini, elimu imekufa na viongozi wanasomesha watoto wao shule za private, ujenzi holela mijini bila town planning inayoeleweka, kiongozi wa serikali anakuwa tajiri mkubwa katika kipindi kifupi tu, viongozi wanatibiwa nje ya nchi na walalahoi maji safi hawana, n.k., .......... Je hili ni taifa la watu wa namna gain?????. Taifa stars ni sehemu ya hii jamii ya taifa la under-performers, it's not their fault.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...