Umoja wa Watanzania ujerumani(UTU) kwa kasi kubwa inaiwakilisha vema Tanzania huko Ughaibuni,kwa kutumia nafasi zote wanazopewa nchi Ujerumani, ni juzi kati tu Umoja huo ulishiriki katika maonyesho ya "Brüderschaft der völker " mjini Aschaffenburg, ambapo wageni wengi walivutiwa sana na shughuli za Umoja huo za kuitangaza Tanzania, Umoja wa watanzania ujerumani (UTU) unatilia mkazo sana katika kuwashawishi wadau wa kimataifa wawekeze katika udumua za jamii kama vile Elimu,Afya n.k Umoja huo umepokea mialiko ya kushiriki maonyesho mengine yakiwemo makubwa kama International African Festival Tubingen 2013 yatakayo anza 8 hadi 11.08.2013 usikose kuwasiliana nao at kamati.utu@googlemail.com
baadhi ya watanzania na marafiki zao ujerumani.
wadau wa UTU wakiwa katika moja ya maonyesho ya Aschaffenburg.
Mdau
baadhi ya bidhaa katika banda la UTU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. mwenyekiti Mfundo, tunaomba picha zinazoonekana vzuri. Mbona mlipiga picha nyingi nzuri tu zilizokuwa zinaonekana vizuri

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2013

    mwingine ana bendera ya Kenya! Anawakilisha Kenya nadhani.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2013

    Mimi nimeona mwenye Bendera ya Uganda.

    Sasa sielewi maana watu wakiwa Majuu Wana Afrika ya Mashariki nchi zote 5 Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda HATA ZINGINEZO kama Congo DRC,Malawi, Zambia,Msumbiji,Ethiopia na Somalia ili mradi wanaongea ama wanaelewa kiasi kidogo Lugha ya Kiswahili hujisikia kama ni Sehemu ya Tanzania!

    Licha ya hilo, hawa ndugu zetu baadhi yao wa nchi hizo wamekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Watanzania kama ndugu sehemu mbali mbali Duniani.

    Mungu Ibariki Afrika , Mungu Ibariki Tanzania!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2013

    Lakini Rwanda MMMMMMMMMMMMMMM!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 29, 2013

    Aliyevaa fylana ya Uganda ni kuwa Rangi za Bendera ya Ujerumani na za Bendera ya Uganda ni sawasawa.

    Rangi NYEKUNDU, NJANO NA NYEUSI.

    Hivyo kwa kuwa Uganda ni sehemu ya Afrika ya Mashariki Mdau ameona atumie Bendera hiyo ili kuweka u-Pamoja na Wajeruani ili wajisikie wamoja ktk shughuli!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...