Taswira za askari wa jadi wa jimbo la Tyrol huko Alpbach nchini Austia wakiingia kwa gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima ya Rais Jakaya Kikwete aliye katika mkutano wa Kamisheni ya Ulaya mjini humo. Historia ya askari hawa, wanaojulikana kama Schuetzenkompanie, inakwenda miaka ya 1810 wakati wa vita na watu wa Bavaria. Soma historia yao BOFYA HAPA
 Sungusungu hao wakiendelea kuwasili
 Kila mmoja ana gobole lililotengenezwa kienyeji
 Watoto kwa wakubwa wamevutiwa na Sungusungu hao
 Gwaride rasmi
 Mdau anajiunga na Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Austria Mhe Heinz Fischer (katikati), Rais wa Kamisheni ya Ulaya Mhe Jose Manuel Barroso (wa pili kushoto), Rais wa Mkutano wa Alpbach Dr Franz Fischer (kushoto) pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandala

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Duhhh Dunia kijiji!

    Ina maana Tanzania sisi kuwa na Sungusungu kuanzia huko Magu na Kwimba hadi Mijini kama Dar tuliona mbali mwanawane.

    Yaani haya mambo huku Tanzania tunayadharau kumbe Majuu yapo?

    ReplyDelete
  2. Mugambo ni Sungusungu?
    Wajameeni kumbe na wazungu na wao washilumu

    ReplyDelete
  3. Duh!Kumbe sungu sungu wapo hadi Ulaya?

    ReplyDelete
  4. Huyu mdau kachomokea wapi peku? Duh haka kataajiriwa kabla ya kumaliza shule.

    ReplyDelete
  5. Hahahahah!

    Wadau hapo juu,

    Halafu wewe hapo Mtaani kwako ukipangiwa ulinde Sungu sungu usiku kucha na Mjumbe wa nyumab 10 unakuja juu na unakwepa zoezi hilo muhimu kwa usalama wako!!!

    ReplyDelete
  6. Si mchezo ndio maana Wasukuma na Wanyamwezi nchini Tanzania wanaitwa Wamarekani na Wazungu wa Kiafrika!

    Si mmeona mambo yao ya Usungusungu hata Majuu yapo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...