Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando(katikati) akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure ijulikanayo kama Hakatwi mtu hapa, itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure popote pale nchini. Kushoto Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa (kulia) Meneja masoko Airtel money Rwebu Mutahaba.
Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa akiongea na wahandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure itakayo wawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure, pichani Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando.
Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando na Meneja masoko Airtel money Rwebu Mutahaba kwa pamoja wakionyesha Bango la hakatwi mtu wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure ijulikanayo kama Hakatwi mtu hapa, itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure popote pale nchini.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa huduma za mawasilino leo imezindua ofa kabambe kwa watumiaji wa huduma ya kifedha ijulikanayo kama ‘Hakatwi mtu hapa’ inayowawezesha wateja wake nchi nzima kutuma na kutoa pesa kupitia huduma ya Airtel money bila makato yoyote.

Promosheni ya Airtel money Bure itatoa unafuu wa kiuchumi kwa wateja wengi wanaotumia huduma ya Airtel money.

akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando alisema “Airtel inaongoza kwa huduma bora zenye gharama nafuu nchini, na tunaendelea kutoa huduma zenye ubunifu kwa kuzindua promosheni mbalimbali kwa mwaka mzima.’Hakatwi mtu hapa’ promosheni tunayozindua leo ni mfano na mwendelezo wa dhamira yetu ya kufanya huduma ya Airtel money kuwa suluhisho na huduma bora ya kifedha nchi nzima”.

Kwa upande wake Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa aliongeza kwa kusema “ promosheni hii itawawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma na kutoa pesa kwenye mtandao wowote bila makato.

“Tunayofuraha kuweza kutoa unafuu kwa wateja kufanya miamala ya pesa bila makato yoyote na kuwaondolea gharama za kutuma na kutoa fedha zillizokuwepo hapo awali. Tumeamua kufanya hivyo ili kuwawezesha wateja wetu kupata kiasi chote cha pesa zao bila makato yoyote” aliongeza Singano.

Airtel kwa sasa inaendesha promosheni maalumu kwa wateja wake ya Airtel yatosha. promosheni ya ‘Hakatwi mtu hapa’ ni msisitizo unaoonyesha Airtel yatosha ambapo huduma zote ikiwa ni pamoja na kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi, huduma za internet na sasa kwenye huduma ya Airtel money ambayo inakuwa promosheni kabambe , nafuu kuliko zote nchini. Huduma ya Airtel money sasa bila shaka Yatosha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...