Mkufunzi toka taasisi ya Risxcel, Sunny Ahonsi akitoa mada kuhusu Governance and Parliament kwa viongozi wa Bunge.Naibu Spika Job Ndugai (kwanza kushoto), Wenyeviti wa Bunge (Mhe Zungu na Mhe Mohamed Seif Khatib) wako Dubai katika mafunzo maalum kwao kama viongozi wa Bunge wakiongezewa uwezo katika maeneo ya Uongozi Bora, Uendeshaji wa Vikao na Mikutano na tathmini ya mifumo na uongozi wa kibunge duniani.Mafunzo hayo yanatolewa na jopo la wataalamu toka Uingereza kupitia taasisi ya Risxcel.
Mhe Job Ndugai akitoa maelezo kwa wenzake juu 'Leadership Values', Mafunzo hayo ambayo ni ya vitendo zaidi ni sehemu ya mipango ya Ofisi ya Bunge kuongeza ujuzi kwa
wabunge na viongozi wake.
Mhe Zungu akichangia katika moja ya mijadala kwenye mafunzo hayo.
Viongozi wa Bunge wakiwa katika mazoezi ya vitendo juu ya Uongozi.Kushoto ni Bi.Maria toka Uingereza akiendesha zoezi la 'Leading by Example. Picha na Saidi Yakubu.
Baada ya hayo mafunzo wakipewa jaribio 60% watapata Div 0, bisha!
ReplyDeleteKwetu sisi mafunzo na vitendo tofauti kabisa. Injinia hawawezi kufanya mambo kama ujenzi, Spika hawezi kuacha unazi, Prof. wa uchumi hawezi kubadili uchumi, ..... yaani listi ni ndefu.
ReplyDeleteDiploma, Degree, Semina, Kongamano, warsha, ziara za mafunzo hazileti mabadiliko kwetu hapa Tanzania.
Mdau
Makini
Sibishi kabisa mtu wangu,naungana na wewe
ReplyDeleteHaaaaah!Hii kali....na mahasira yao yatawekwa wapi?
ReplyDeleteInashangaza . Lakini ni vema mchawi ukimkabidhi mtoto