Na Abdulaziz Video,Dodoma
WAKULIMA wa zao la korosho nchini wametakiwa kubadili mitazamo yao
kuona zao hilo kuwa la kudumu badala ya kuliona la kujikimu kwa muda
na kusababisha kushuka kwa uchumi wao, na kuendelea kuwa masikini,
kila mwaka.
Hayo yamebainishwa na waziri wa Kilimo, chakula na ushirika Mhandisi
Christopher Chiza wakati alipokuwa anafungua mkutano wa wadau wa
korosho wa siku mbili ulifanyika mjini Dodoma.
Chiza aliyasema hivi sasa za la korosho linazidi kupanuka kiuzalisha
kwa kuongezeka kutoka wilaya 34 hadi 41 na mikoa tisa mipya
inayolima zao hilo Mbeya, Iringa,Njombe, Morogoro,Dodoma Singida
Alisema kuwa zao hilo bado halijaweza kutoa tija kwa wakulima, kwa
hiyo aliwataka watendaji kutumia vyema kikao hicho kujadili kwa kirefu
juu kuleta mabadiliko kwa wakulima na kuondokana na umasikini.
Waziri Chiza alifananisha na mazao mengine ya kudumu kama, Kahawa,
migomba ya ndizi, Pamba ambayo yaliweza kuleta sura nzuri ya kiuchumi
kwa wakulima wa mazao hayo.
Hata hivyo aligusia swala zima la ubanguaji wa zao la Korosho, kuwepo
na jopo maalumu ambalo litaweza kukaa pamoja na kuhakikisha zao hilo
linabanbuliwa nchini.
Aliongeza korosho inayosafirishwa ghafi inasababisha hali ya wakulima
kuendelea kuwa masikini.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Anna Abdallah alisema kuwa
viwanda bado vinashikiliwa na wafanyabaishara wabangue hapa hapa
nchini.
Alisema kuwa korosho ghafi soko lake liko sehemu moj tu ni nchini
india jambo linalosababisha kuleta mgongano wa kimaslai kati ya
wanunuzi watendaji wa sekta ya ushirika na walimu
Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika,Eng. Christopher Chiza akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa korosho wa siku mbili ulifanyika mjini Dodoma.
Baandi ya Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
Tatizo sugu la Kihistoria nchini Tanzania lipo katika Mfumo wa Masoko ya mazao ya Wakulima:
ReplyDelete(i)-BODI ZA MAZAO:
1.Kahawa,
2.Korosho,
3.Pamba,
4.Chai,
5.Pareto,
(ii)-HALMASHAURI:
(iii)-WADAU NA MADALALI (vishoka):
Serikali ivunje Udhalimu huo hapo juu (REGIME) ndio mambo yaweze kuwa mambo kwa Wakulima.
Sasa kutokana na Mfumo huo hapo juu Dhalimu wa 'KARATA TATU' (i), (ii) na Masoko (iii) ndio sababu Mkulima anazidi kuwa Masikini hivyo kulichukulia zao kama la kumpatia Tija ya muda tu ambapo kilimo kinakuwa ni cha kujikimu na si kama Biashara!!!