THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WATUMISHI WA IDARA YA WAKIMBIZI WAMUAGA RASMI ALIYEKUWA MKURUGENZI WA IDARA HIYO, JUDITH MTAWALI, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Judith Mtawali (kulia) ambaye amestaafu rasmi kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma akikata keki wakati wa sherehe iliyoandaliwa na watumishi wa Idara ya Wakimbizi kwa ajili ya kumuaga na kumtakia maisha mema yenye mafanikio maishani mwake. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Michokeni Resort Centre, jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Idara ya Wakimbizi wakipeleka zawadi zao kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Judith Mtawali ambaye amestaafu rasmi kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Michokeni Resort Centre, jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Judith Mtawali ambaye amestaafu rasmi kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma akizungumza kwa furaha kwa kuwashukuru watumishi wa Idara ya Wakimbizi kwa zawadi nyingi walizompa pamoja na kumtakia heri maishani mwake. Aidha, Mtawali aliwaomba watumishi hao waendelee kufanya kazi kwa uadilifu na hatimaye watakuja kufanikiwa maishani mwao. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Michokeni Resort Centre, jijini Dar es Salaam.
Watumishi wa Idara ya Wakimbizi wakichukua chakula katika hafla hiyo iliyofanyika kwa ajili ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Judith Mtawali ambaye amestaafu rasmi kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Michokeni Resort Centre, jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Judith Mtawali (katikati waliokaa) ambaye amestaafu rasmi kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa idara hiyo mara baada ya kupokea zawadi mbalimbali kutoka kwa watumishi hao. Kulia (waliokaa) ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo, Harrison Mseke. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Michokeni Resort Centre, jijini Dar es Salaam. (Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).