Baadhi  ya wahitimu wa  darasa la saba shule ya Southern Highlands Mafinga mwaka 2013
mkurugenzi mtendaji  wa shule ya Southern Highlands Mafinga Iringa Bi Mary A. Mungai akiwahakikishia  wazazi ubora wa shule  yake
mkurugenzi mtendaji  wa shule ya Southern Highlands Mafinga Iringa Bi Mary A. Mungai akimpongeza mmoja kati ya  wahitimu wa  darasa la  saba mwaka 2013.

Na Francis Godwin Blog

WAKATI wanafunzi wa darasa la saba kote nchini wakiendelea kusubiri matokeo ya mtihani wa darasa la saba ,uongozi wa shule ya kimataifa ya Southern Highlands Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani hapa umewahakikishia wazazi kuwa wawe na uhakika mkubwa wa watoto wao kufaulu mtihani huo.

Mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Bi Mary Mungai ambae amepata kuwa afisa elimu wa shule za msingi alitoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya 13 ya darasa la saba shuleni hapo juzi.

Alisema kuwa toka shule hiyo ilipoanzishwa mwaka 1994 kama Day Care na Pre-school na mwaka 1997 kuanza shule ya msingi imekuwa ikifanya vizuri na hakuna mtoto aliyepata kufeli .

“Shule yetu mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanza wa darasa la Saba na wanafunzi walikuwa 17, wote walifaulu vizuri na wote walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza” Alisema katika matokeo ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 Southern Highlands School ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani ya Somo la Kiingereza. 

“ Tulimshukuru Mungu na tunaendelea kumshukuru Yeye. Kwa kuwezesha watoto wetu wa Southern Highlands School, kufaulu vizuri, kwa kishindo” alisema Bi Mungai Hata hivyo alisema kila wanafunzi wote wamekuwa wakifaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na wote kuchaguliwa na kuendelea na masomo ya Sekondari.

“Ninaamini wanafunzi wote wa darasa la saba 47 waliomaliza mwaka huu 2013, watafaulu na kuchaguliwa kuendelea na sekondari….. Sababu walikuwa wanapenda masomo na nidhamu yao ni nzuri.”

Kwa upande wake mkurugenzi wa bodi ya shule hiyo Bw Omary Mahinya alisema kuwa katika moja ya vielelezo kuwa shule hiyo ni bora nchini ni wazazi kutoka mikoa karibu yote ya Tanzania kupeleka watoto wao hapo .

“Wahitimu toka shule yetu wamekuwa wakifanya vizuri katika Sekondari kidato cha IV na kidato cha VI popote walipo kwenda… hii inadhihirisha kuwa Southern Highlands School imewajengea msingi bora wa Elimu ambao ni TUNU ya kujivunia sana. Aidha alisema kuwa lengo la uongozi wa shule hiyo ni kuhakikisha kuwa Southern Highlands School inakuwa mfano bora na kioo kwa jamii inayotuzunguka kwa kuweka mazingira bora ya kuishi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. kiukweli ni shule nzuri sana..na kama anavyosema inawajengea watoto msingi mzuri wa kielimu..nasema hivi kwa 7babu nimesoma hapo,nimemaliza form 6 sasa..najua"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...