Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kifungo cha miaka saba jela washitakiwa katika kesi ya wizi wa Sh bilioni 1.1 fedha za Epa.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Bahati Mahenge, Manase Mwakale, Davies Kamungu, Godfrey Mosha na Eda Mwakale. 

Washitakiwa waliotiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo kati ya hao watano ni Bahati mahenge (kifungo cha miaka 7 jela), Manase Mwakale (miaka mitano jela) na mke wake eda Mwakale (miezi 18 jela) huku washitakiwa waliobaki kuachiwa huru.

Washitakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashitaka tisa ambapo mashitaka saba walikutwa na hatia nayo na mashitaka mawili ambayo ni ya wizi na kujipatia ingizo kuondolewa na mahakama baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuyafanyia marekebisho wakati wa ushahidi wao.

Haikuwa ni jambo la kupendeza, majonzi yalitanda mahakamani kwa ndugu na jamaa wa washitakiwa hao baada ya kuona wapendwa wao wameamuriwa kwenda kuanza kuishi maisha ya kifungoni, mbali nao.

Mashitaka yaliyokuwa yakiwakabili ni pamoja na kula njama, kutoa hati ya kiapo iliyoghushiwa, kusajili kampuni kutumia nyaraka feki, kughushi hati ya umiliki wa deni hilo, kughushi hati ya makubaliano, wizi na kujipatia ingizo.

Ilidaiwa kuwa kati ya mwaka 2004 na 2005, washtakiwa waliiba na kujipatia kwa njia ya udanganyifu fedha hizo kwa kutumia kampuni ya Changanyikeni Residential Complex Ltd ya Tanzania wakidai wanakusanya madeni ya kampuni ya Marubeni Corporation ya Japan.

Ilidaiwa kuwa washtakiwa kwa kutumia nyaraka za kughushi, walijipatia ingizo la hilo baada ya kudanganya kuwa Kampuni ya Changanyikeni Residential Complex Ltd imehamishiwa deni na Kampuni ya Marubeni Corporation.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...