Watanzania nchini Uingereza wamejitayarisha kuhudhuria mkutano wa wazi siku ya Jumamosi mchana ili kumsikiliza Mbunge wa Iramba Magharibi Ndugu Mwigulu Nchemba. Huu ni mwendelezo wa ziara alizofanya Ndugu Nchemba na ujumbe wake akitokea Marekani alipopokewa na mamia ya watanzania na makada wa CCM nchini huko.

Aidha katika ziara zake nje ya nchi ndugu Nchemba ameweka bayana msimamo wa CCM na Serikali yake katika hatua za makusudi za kuhakikisha watanzania nje ya nchi wanatambulika katika mipango madhubuti ya kitaifa na kwamba wakati umefika wa rasilimali za wanadiaspora kuanza kutumika kujenga nchi yao bila uwoga.

Uchunguzi wetu umefanya mawasiliano na kubaini kuwa watanzania toka majiji mbalimbali ya hapa Uingereza watasafiri kuhudhuria mkutano huo ili kujua serikali imeandaa mbinu gani mpya za kutatua kero za watanzania wanaoishi diaspora. Mkutano huo ambao utaambana na meza ya vyakula na vinywaji itakayoandikwa na mpishi maarufu wa kitanzania na baadaye kufuatiwa na muziki utafanyika katika ukumbi maarufu na wa kisasa wa St. Patrick's 100, Beaumont. Leys Lane. Leicester. LE4 2BD.

Na Leyla Shomari,
Tanzania Now: Freelance Observers: Slough. St.Marys Road. SL3

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. na kwa wingi wetu tunakwenda.Tanzania ni moja.

    Maafudh Seif.

    ReplyDelete
  2. CCM UK INAWAKARIBISHA WATANZANIA WOTE , Wanachama na Wasio Wanachama katika Mkutano huu . Kama Watanzania wa nje ya NChi , nia yetu ni moja katika kuhakikisha tunapeleka mchango wetu wa hali na mali nyumbani katika kuendeleza nchi. Karibu umsikie Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Siasa, usingoje kuhadithiwa akikueleza nini kinafanyika kwenye utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Serikali ya CCM. CCM OYeee

    Mariam M
    KATIBU CCM UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...