Rais  Kikwete na Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakiwa na makamanda na viongozi katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
 Rais Kikwete na Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani wakiwa na wakuu wa vyombo vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani
 Rais Kikwete akiongea na Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani na wakuu wa vyombo mbalimbali vya dola vilivyo chini ya wizara ya mambo ya ndani
 Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani akiwa na viongozi wa vikosi mbalimbali vilivyo chini ya wizara yake
Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA Naibu Waziri wa Fedha na Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb) Naibu Waziri wa Fedha na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya fedha. PICHA NA IKULU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Waheshimiwa mliokuwa "wateule" hapo jana na sasa mkiwa na nafasi kamili (NWs) mmependeza katika picha si ndiyo bwana, tena mko na wapambe hapo - wamefurahia ujio wenu katika Wizara hiyo nyeti.....lakini sasa kupendeza huko katika picha kwende pamoja na matarajio ya Muheshimiwa Rais JK kwenu....fanyeni kazi waheshimiwa si mmesoma hapo jana Muheshimiwa JP. Magufuli wakati balaza linatangazwa yeye yuko kugagu ujenzi wa daraja la Kigamboni....yaani kwa tafsiri ya haraka haraka maana yake ni kwamba mara baada ya Ibada/Misa ya JPili (hapo jana) Muheshimiwa Magufuli aka-unga moja kwa moja kibaruani; yaani kama ni sabato & torati basi Magufuli alikwenda zaidi ya umbali wa kutupa jiwe (acha hayo)

    Tuje kwenu: sasa na nyie waheshimiwa pigeni kazi bwana acheni kumpa wakati mgumu Muheshimiwa Rais JK, unajua uzembe wowote katika utendaji wenu maana yake mmnaudhalilisha uteuzi wa Muheshimiwa Rais (hiyo ndo manake)....mpeni raha JK fanyeni kazi kwa weledi, kwanini mnataka amalizie kipindi chake kwa kuumiza kichwa juu ya watendaji dhaifu?

    ReplyDelete
  2. Tunategemea mtampa Ushirikiano Raisi Kikwete ili tulisukume gurudumu la maendeleo na Tanzani kusonga mbele!

    Baada ya kula Kiapo kinacho fuata Siasa Pembeni Taifa kwanza!!!

    ReplyDelete
  3. Msimwangushe Raisi JK tafadhali ili naye atimize ahadi zake kwetu Wananchi!

    Ni vile maendeleo ya nchi hayaletwi na mtu mmoja pekee bali Timu ya watu wenye nia njema, walio dhamiria na Mfumo mzima.

    Isingekuwa hilo ili kuondoa lawama na fitina Raisi Jakaya Kikwete angeshikilia Wizara zote na Idara zote Muhimu na kufanya kazi peke yake!

    Lakini kwa kuwa kama nilvyosema mambo yanaendeshwa na (i)Timu ya watu wenye nia nema na dhamira, (ii)Mfumo wa Utendaji, ndio maana tunakuwa na Utamaduni huu wa kuaminiana(ndio maana pana Kula Kiapo) na kuchaguana ili kubeba dhamana pia Majukumu na kuendesha mambo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...