Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea barua kutoka kwa Mhe. Spika wa BUNGE la Jamhuri ya Muungano Tanzania ya kuiarifu uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Kalenga lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Vijijini, kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. William Mgimwa aliyefariki dunia tarehe 1/1/2014. Baada ya taarifa hiyo Tume imepanga ratiba ya Uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kalenga kama ifuatafyo:-

1.     Uteuzi wa Wagombea Ubugne utafanyika tarehe 18-Februari-2014 
2.     Kampeni za Uchaguzi zitaanza tarehe 19-Februari-2014 hadi 15-Machi-2014 
3.     Siku ya kupiga kura ni Jumapili terehe 15-Machi-2014 
Wagombea wanatakiwa kuwasilisha Fomu za Uteuzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi wa JImbo la Kalenga siku ya Uteuzi si zaidi ya Saa 10:00 Alasiri. Tume inawataarifu Wananchi wote pamoja na Vyama vya Siasa kufuata ratiba iliyotolewa pamoja na kushiriki katika mchakato mzima wa Uchaguzi kuanzia siku ya Uteuzi hadi siku ya Kupiga Kura ili watimize haki yao ya Kikatiba ya Kuchagua viongozi wanaowataka.

Tume inawasisitiza wananchi wote katika maeneo husika kujitokeza kukagua taarifa zao wakati wa kuweka wazi Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuona kama kuna marekebisho madogo yanahitajika kufanyika kuwawezesha kupiga Kura bila malalamiko yoyote. Ikumbukwe kwamba hakutakuwa na uandikishaji mpya wa Wapiga Kura.

J. Mallaba
MKURUGENZI WA UCHAGUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tunashukuru kwa taarifa, ila naona tarehe hapo zimegongana. Kampeni zinamalizika tarehe 15 machi na uchaguzi jumapili tarehe 15 machi. Jumapili ni tarehe 16 na sio 15.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...