Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa wenyeji wake kuhusiana na ujenzi wa hatua za awali za bandari ya Kabwe,wilayani Nkasi mkoani Rukwa.
 Katibu Mkuu wa CCM;ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kirando,wilayani Nkasi mapema jana jioni.Kinana alisema kuwa tahakikisha Barabara ya kutoka Sumbawanga mjini kwenda kijiji cha kabwe itatengenezwa kwa kiwango cha lami."Nitaenda na mbunge wenu kushinikisha suala la barabara hii ili ijengwe kwa kiwango cha lami na kuwarahisishia sughuli za  kibiashara"alisema.Alisema kuwa maendeleo hayawezi kuja ikiwa miundombinu ni mibovu hivyo atahakikisha analifikisha kwa waziri mwenye dhamana pamoja na mkuu wa nchi ili kazi hyo ifanyike mapema. 

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wananchi na wanachama wa CCM,mapema jana jioni katika kijiji cha Kabwe,Wilayani Nkasi.Kinana alisema kuwa, Serikali inatambua  matatizo ya wananchi wa kjijini hapo ikiwemo suala la pembe jeo, maji pamoja na uvamizi wa wavuvi. "Miradi yote inayotekelezwa nchi nzima kwa sasa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010, hatubagui kwakua wote ni watanzania"alisema.Alisema kuwa Serikali inatambua kuwa shughuli kubwa ya kijini hapo ni uvuvi hivyo itajitahidi kuwe na utaratibu wa kuwasaiidia kupata mikopo ili waweze kununua zana za uvuvi ili waweze kujiendeleza.
 Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akiangalia samaki katika kiwanda kidogo cha kuhifadhia samaki na kuuza katika kijiji cha Kabwe,Wilayani Nkasi mkoa wa Rukwa  mapema leo,ambapo pamoja na mengine Ndugu kinana alifanya mkutano wa hadhara ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 21 katika mikoa ya Rukwa,Katavi na Kigoma,ziara hiyo ikiwa na lengo la kuimarisha Uhai wa chama,kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata ilani ya CCM.
 Samaki aina ya Migebuka ikiwa imeandaliwa kwa ajili ya kukaushwa kabla ya kuhifadhiwa kwenye majokofu  na kusafirishwa maeneo mbalimbali,ndani na nje ya nchi.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo na  Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini,Mh.Ally Keisy alipokwenda kukagua ujenzi wa bandari ya Kabwe katika hatua za awali  na kujionea shughuli mbalimbali za uvuvi zinazofanyika katika kijiji hicho kabwe.
 Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM katika kijiji cha Kabwe,wilayani Nkasi mkoani Rukwa mapema leo jioni.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...