Tatizo la muda mrefu la uhaba wa maji ya uhakika linalowakabili wakaazi wa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa mengine inayohudumiwa na mitambo ya maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini sasa litakuwa historia...
 Mafundi wakiendelea kulaza mabomba yatakayotumika kusafirishia maji kutoka Mitambo ya Maji ya Ruvu Chini mpaka kwenye Tanki la kuhifadhia maji lililopo Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa mafundi hao wameshasambaza mabomba kwa umbali wa kilomita takribani 29 kati ya kilomita 55. Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, mwaka huu.
 Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Watatu kushoto) kwenye lenye uwezo wa kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa siku wakati walipokuwa kwenye ukaguzi wa  mitambo ya Ruvu Chini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...