THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

HIVI NI KWELI HAPA PAMESHINDIKANA??

 Ni Miaka mingi sasa imepita huku shimo hilo la chemba likifanyiwa vibweka vya kuwekewa mavitu ya aina mbali mbali ikiwa ni ishara ya alama kwamba hapa kuna shimo.kiukweli shimo hili ni kero sana kwa watumiaji wa njia hiyo hasa ukizingatia lipo maeneo ya katikati ya jiji la Dar pembeni ya jengo refu la Benjamin Mkapa Tower na usoni kwa Makao Makuu ya Benki ya NMB.swali linakuja,hivi ni kweli kwamba hapa pameshindikana kufanyiwa kabisa kutafutiwa ufumbuzi yakinifu?


Kuna Maoni 4 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Jamani Manispaa, mnatumia muda mwingi kukimbizana na Wamachinga Jijini huku mkitoza Wafanya biashara ada nyingi tu.

  tunapokea Mabilonea wa Dunia wakija Bongo kwenye Utalii zibeni mitaro hiii haraka sana!

 2. Anonymous Anasema:

  Kweli haya ni maajabu. Viongozi wenye dhamana wanasubiri wawekezaji waje wazibe hili shimo. Vitu vidogo kama hivi vinatosha kurudisha nyuma mazingira ya uwekezaji. Sisi tunakimbilia kutoa misamaha ya kodi. Viongozi wa jiji bwana wanafurahisha. Uchafu kibao. Jiji linafagiliwa kwa fagio la mti!!!!!

 3. Anonymous Anasema:

  Kama vyuma vinaondolewa na watu wa vyuma chakavu, zibua chemba uweke mifuniko ya zege, kuweka kisiki ni kwa ajili ya kuonya watumiaji wa barabara.

 4. Anonymous Anasema:

  Jamaa hawachelewi kusingizia diaspora, inagwa hatupo kwenye uchaguzi wa vingozi wao.