MASHINDANO ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii inayowahusisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari (NSSF Media Cup) yameanza kutimua vumbi katika uwanja wa TCC, Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Akifungua mashindano hayo, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka, amewataka wanahabari nchini kuhakikisha wanajiunga na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ili kujihakikishia maisha ya amani na utulivu baada ya kustaafu.

Alisema kuwa, wanahabari wanapaswa kwenda mbali zaidi katika kulitumia shirika hilo, ili kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa kwa wanachama.

Katika ufunguzi huo, timu ya soka ya New Habari (2006) Ltd iliumana na Habari Zanzibar katika Soka, ambako hadi  filimbi ya mwisho Habari Zanzibar iliibuka kidedea kwa magoli 4-1, magoli ya Zanzibar yaliwekwa wavuni na Amoor Suleiman aliyeweka wavuni goli moja na Yusuph Juma magoli matatu huku goli la New Habari likiwekwa wavuni na Florian Mwasinde.

Kwa upande wa netiboli, timu ya Jambo Leo iliichapa timu ya Wizara ya Habari Bara kwa jumla ya magoli 59-8, katika pambano la upande mmoja lilipoigwa kwenye viwanja hivyo.

Katika mechi ya pili ya netiboli, Azam Media iliumana na Tanzania Standards Newspaper (TSN), ambako Azam waliibuka washindi kwa magoli 18-13.

Kabaka aliwataka washiriki wa mashindano hayo ya 11 yanayoshirikisha wafanyakazi wa vyombo vya habari kuonesha ushindani, ufundi na nidhamu ili kuongeza hamasa ya michuani hiyo.

Alivitaka vyombo vya habari kuepuka kuingiza wachezaji wasio wanahabari (mamluki), kudumisha lengo la umoja na ushirikiano baina ya shirika hilo kongwe na vyombo vya habari, ikiwamo kuwapa mazoezi wafanyakazi wa vyombo hivyo.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Chiku Matesa.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Carolyne Newa wakati alipotemberlea banda la NSSF wakati wa uzinduzi wa mashindano ya NSSF Media Cup 2014 kwenye uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akisalimiana na mshambuliaji wa timu ya New Habari 2006, Joh Dande wakati wa uzinduzi wa michuano ya NSSF Media Cup 2014 kwenye uwanja wa TCC Chang'ombe Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...