ALIYEKUWA Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Mei 4 Jijini Mwanza.Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti  wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Abihudi Mang’era kamati imejipanga  kufanya tamasha la kishindo jijini humo kwa sababu maandalizi yake ni ya hali ya juu.

Mang’era alisema tamasha hilo litakuwa ni la aina yake ambako alitoa wito kwa wakazi wa Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo. Mang’era alisema sambamba na Ngeleja, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele anatarajia kuwa mgeni rasmi mkoani Shinyanga Mei 3. Aidha Mang’era  alisema mipangilio ya kuelekea tamasha hilo inaendelea vizuri hivyo wakazi wa Kanda ya Ziwa wakae mkao wa kula kupata neno la Mungu kupitia waimbaji mbalimbali wa Tanzania na nje.

Alisema tamasha hilo jijini Mwanza linatarajia kukongwa na muimbaji raia wa Afrika Kusini, Rebecca Malope na wengineo watakaoteuliwa na kamati ya maandalizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...