THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

NSSF yatambulisha bima ya ''WESTADI'' kwa watanzania waishio Ughaibuni

Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza ukishirikiana na Urban Pulse Creative Media wanakuletea ziara ya Raisi Jakaya Kikwete London Tarehe 30.3.14 kukutana na watanzania waishio uingereza.

Kabla ya kuwasili kwake mh Rais shirika la NSSF lilipata fursa ya kutambulisha bima ya ''WESTADI'' kwa watanzania wote waishio Ughaibuni ili kuwawezesha kupata unafuu wa kusafirisha mwili au mazishi pale popote alipo mara anapofariki ughaibuni. Pia Bima hio kusaidia matibabu kwa ndugu na jamaa kadhaa nyumbani.


Kuna Maoni 3 mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Ndg Mashaka, hakika ni Lulu ya Tanzania. Hata tofauti na Nyerere au Dr. Slaa

  2. Anonymous Anasema:

    Ndugu zangu wa Urban Pulse mkumbuke kuwa sisi wa huku internet tunalipia kwa MB kwahio tunaomba msirembe sana, wekeni vitu straight to the point ukizingatia net yenyewe 128kbps!

  3. Clara Anasema:

    Je, nikitaka kujiunga na mpango wa WESTAD, na ninasoma huku Marekani na ninapaswa kununua health insurance kila mwaka kwa $1,567 ni siwezi kupata hiyo ninaweza kupata $300 kwa mwaka za kujiunga na mpango huo naweza kutumia mpango huo nikiwa huku Marekani? naomba ushauri wenu watanzania kwani nami ni mtanzania wa Marekani, mwanafunzi.